Mchezaji Mpira Avunjiwa Mkataba Baada ya Kugundulika Ana Virusi vya Ukimwi

Zikiwa zimepita siku nne tu tangu asajiliwe na klabu ya Al Ittihad inayoshiki ligi kuu ya Misri, Samuel Nlend, 21, mkataba wake umevunjwa baada ya klabu yake mpya kugundua mchezaji huyo anamaambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Jarid linalojulikana kwa jina la KingFut.com limeripoti kuwa, afisa habari wa klabu hiyo amethibitisha taarifa hiyo ya kusikitisha kwa vyombo vya habari.

Mshambuliaji huyo ameitumikia Cameroon katika michezo mitano, alifunga goli January kwenye michuano ya mataifa ya Afrika kabla ya kujiunga na Al Ittihad majira ya kiangazi.

Samuel Nlend alisaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Al Ittihad tangu tarehe 24 August. Licha ya hayo yote kutokea bado amepata support ya kutosha kutoka kwa klabu yake mpya ya Misri.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mbona ukimwi haujamzuia kufunga magoli?

    ReplyDelete
  2. Wanamichezo wengi wa kiafrika wakipimwa ( vipimo vya kweli.) Basi Afrika hatutakuwa na wachezaji wengi.

    ReplyDelete
  3. Hilo ni kosa kubwa sana kusambaza ugonjwa wa mtu au afya ya mtu hasa kuhusu ugonjwa wa ukimwi katika social media hata daktari haruhusiwi kumwambia mtu yeyote zaidi na yule aliyepima hospital kuna kile kitu kinaitwa secretess hasa ukipimwa ugonjwa huo sababu hamna mtu anayetaka mtu mwingine ajue kuwa anasumbuliwa na ugonjwa huo kama nchi za ulaya daktari haruhusiwi kutoa siri kama hiyo ila kama unao ugonjwa huo na unajijua halafu unawaambukiza watu makusudi na ushahidi upo ndiyo hapo watakuanika kwenye social media na taarifa za habari na vile vile utakamatwa na kufungwa jela miaka mingi sana hapa ulaya wengi wamefungwa kwa makosa hayo ya kuambukiza watu halafu kama mtu ni muhamiaji utafungwa jela ukitoka jela unarudishwa kwenu. Lakini huyo mchezaji wa mpira hajamuambukiza mtu lakini wanamuanika katika social media hilo ni kosa kubwa sana anaweza kuwashitaki FIFA hao watu waliomuanika katika social media na hao watu wakafungiwa au kufukuzwa kazi, sababu wameshamuharibia maisha kijana wa watu na bado ana umri mdogo sana kupata matatizo kama hayo yanaweza au yameshamuharibu kisakiolojia

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad