MICHEZO Bilionea anayetaka kuinunua Simba, ametaja kilichomsikitisha katika mkutano wa Simba

Siku moja baada ya mkutano mkuu wa Simba kufanyika na kukubali kupitisha maadhimio ya mabadiliko ya kiuongozi ili klabu iendeshwe kwa mfumo wa hisa, bilionea wa 21 Afrika ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) Mohammed Dewji ameelezwa kusikitisha na taarifa za upotoshwaji.

Mohammed Dewji amesikitishwa kutokana na taarifa zilizotolewa katika mkutano mkuu Simba uliofanyika jana July 31 2016, kuwa yeye ambaye aliomba kununua asilimia 51 ya hisa za Simba kama mfumo ukibadilishwa, hajaandika barua kwa uongozi wala kukutana nao ila amekuwa akiongea kupitia vyombo vya habari kitu ambacho sio kweli.

“Kiukweli nimesikitishwa kwa wanaosema dhamira yangu ya kutaka hisa Simba nimeomba kupitia vyombo vya habari na wala sijaandika barua, ukweli nimekutana na Rais wa Simba Evans Aveva zaidi ya mara tatu, ameshakuja ofisi kwangu zaidi ya mara tatu”

“Kuhusu kuandika barua nilikuwa sijaandika kwa sababu mfumo wa hisa niliokuwa nahitaji ulikuwa haupo sasa utaombaje kitu ambacho hakipo, ila leo baada ya mkutano mkuu kukubali nimeandika barua rasmi kwenda kwa uongozi wa Simba na tayari tumeshaituma”

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. anzisha timu yako acha kuleta uchonganishi kwenye timu baina ya viongozi na wanachama

    ReplyDelete
  2. Mzee kule Kwetu songea Kuna club ya maji maji mabingwa wa 1998. Acha na na simba Njoo wekeza huku. Mwaka tu team yako itakuwa tishio. Mbona bakhresa kaanzisha team na saizi inatisha. Hizi team kongwe zinasumbua sana hawana lolote hapo. Jitoe bro

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuna anachokitaka simba,wee subiri tu.
      Bora ya Manji amakuwa mfadhili kwa muda mrefu yanga lakini huyu wa kukurupuka sasa hivi mmmh-mtaniambia siku moja.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad