Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameliagiza jeshi la polisi mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha kwamba sheria zinafuatwa na kusiwepo kitu kinaitwa UKUTA ili wananchi waendelee na kazi zao kama kawaida.
Akizungumza na kikosi cha kutuliza ghasia katika kambi ya Ukonga Jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa amesema kwa kuwa askari wanafahamu sheria wasisubiri mtu yeyote kuja kuwakumbusha juu ya jambo hilo au maelekezo mengine kwa kuwa Amiri Jeshi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameshaagiza kinachotakiwa ni utekelezaji.
‘’Msisubiri maelekezo yoyote kutoka juu, asiwepo mtu yeyote atafunga duka kwa sababu ya UKUTA nyie ni matrekta hakuna UKUTA unaweza kusimama mbele yenu, mimi kama Mkuu wa Mkoa ninaamini hatutakuwa na vurugu kwenye Mkoa wetu na hatuwezi kuruhusu vurugu kwa kuwa tunajua madhara ya vurugu’’ Amesema Makonda.
Aidha kwa upande wake Kamanda wa Oparesheni Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya amesema jeshi la polisi lipo vizuri na vijana wameandaliwa vizuri na wameandaliwa kuwa tayari siku nyingi na hakuna mtu yeyote atakayethubutu kufanya UKUTA na watakaofanya hivyo watazimwa kabla hawajafanya chochote.
Kamada amewataka wananchi wote Jijini Dar es Salaam kuto jitokeza kwenye oparesheni UKUTA kwa kuwa maandamano hayo siyo halali na watakaojitokeza watapata matatizo yasiyowahusu.
Oparesheni UKUTA ilitangazwa na CHADEMA ikiwa na maana Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania na ikatajwa tarehe Mosi Septemba nchi nzima chama hicho kitafanya mikutano ya hadhara jambo ambalo limepingwa na serikali kuanzia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kufuatia wakuu wa mikoa.
Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda Apiga Marufuku Maandamano ya UKUTA, Awapa Rungu FFU
4
August 06, 2016
Tags
Hili ni tangazo la vita. Na mwenyeruhusa ya kutangaza vita ni raisi peke yake. Watanzania, jihadharini kujitungia sheria zenu bila kufuata katiba za nchi. Kuruhusu FFU kufanya lolote kwa wananchi bila mufikiri madhara au maana ua kauli hizi zinaleta wimbi nzito na giza nchini. Jupata cheo safi, lakini kukitumia cheo vibaya bila kujijua pia ni vibaya. Serikali kuwaachia wakuu wa. Mikoa kudharau vyama vinginr vyote na kukingwa kichama hii ni hatari kubwa. Ni madarska ya jali ya juu yanayohitaji hekima ya hali ya juu, ibada ya hali ya juu. Elimu ya hali ya juu sana.kiongozi anayetuma jeshi la ulinzi kuadhibu watu, ni sawa na kutoa amri ya kuua watu.vijana na harakati ya kupanda ngazi. Demokrasi jamani hii nfio inayosumbua. Demokrasi ni haki ya kila binadamu kupewa usawa.usawa wa kuabudu bila bugudha, kuamini na kutenda kazi bila kujali chama.wenyeviti wa mikoa karibu wote ni ccmna wengi wamepewa sauti ya chama kama serikali, kwa manufaa ya chama chao.wakuu wa mikoa inabidi wawe nutral. Kuhakikisha maendeleo mkoani na si kukandamiza wananchi.
ReplyDeleteEti demokrasia!!! Iko wapi Tanzania? Eti nchi ina AMANI!! Amani gani? Kwanini msiwaache waseme wanachotaka kusema kisha WATANZANIA AMBAO SI MAMBUMBU wakaamua la kufuata? Mtanzania wa leo si wa miaka miwili iliyopita, ameamua na anaweza kuchagua limfaalo. Huyu rais ni kwanini anakuwa rais wa kundi moja?
ReplyDeleteAliyekuambia ni maandamano ya vurugu ni nani Junya wewe?...Watu wanapigania haki ambayo wewe na wanaume zako mnataka kuizima, kwa hiyo kama ni vurugu, ni nyinyi na jeshi lenu ndio mtasababisha. Kenge wewe na Boss wako, hamna akili.
ReplyDeleteSawa kabisa..vurugu Na uvunjifu WA Amani hatuuvumulii Na wala hatutouvumilia..
ReplyDelete