MO Kukabidhiwa Simba SC Hali Bado Tete

Baada ya mkutano mkuu wa klabu hiyo uliofanyika leo katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oyesterbay, ambao ulikuwa na ajenda 10, moja kati ya ajenda hizo ilikuwa ikizungumzia taarifa ya kamati ya maboresho ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo.

Katika ajenda hiyo ndipo lilipojitokeza suala zima la MO ambapo wanachana hao wa Simba zaidi ya 700 waliojitokeza kwenye mkutano huo walitaka bilionea huyo apewe timu hiyo kutokana na hali mbaya ya kiuchumi iliyopo klabu hapo ambapo imekuwa ikijiendesha kwa hasara kila mwaka.
Katika msimu wa 2014/15 klabu hiyo ilifanikiwa kujikusanyia Sh bilioni 2, 096, 721, 493  kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali vya mapato lakini ikatumia Sh bilioni 2,101,100,303 na kujikuta ikidaiwa 4, 378,810.

Lakini pia katika bajeti yake ya msimu ujao wa 2016/17 uongozi huo unatarajia kukusanya kiasi cha Sh bilioni 3, 583, 000,000 kutoka katika vyanzo vyake vya mapato lakini matumizi yake yanatarajiwa kuwa Sh bilioni 4, 411,025, 000, hivyo itakuwa ikidaiwa Sh milioni 828, 025, 000.

Kutokana na hali hiyo wanacha hao waliutaka uongozi huo, kukubali kumpatia Mo timu  kwani wanataka mabadiliko na wamechoshwa na hali hiyo ya ukata wa kila wakati ambao umekuwa ukiwatesa na kuwakosesha amani kila siku.

Hata hivyo uongozi wa klabu hiyo chini ya rais wake, Evans Aveva haukuwa tayari kufanya hivyo licha ya kelele za wanachama hao ambao kila wakati walikuwa wakiimba na kulitaja jina la MO.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ushauri wangu Mo apewe uongozi kama Manji kwanza angalau kwa mwaka mmoja ili tumuone.

    ReplyDelete
  2. HUKO JIMBONI KWAKE MBONA KUMEDODA KISOKA?

    ReplyDelete
  3. KAMA KUNA MWINGINE LABDA LAKINI KWA MO HAPANA.

    ReplyDelete
  4. Lkn MO mmbona anajipangia bei mwenyewe?labda bilioni 20 ndio thamani ya jengo la simba.Na kuna uhakika gani hawezi kuuza hisa zake pale thamani inapoondokea maana yeye ni mfanya biashara.

    ReplyDelete
  5. Wapi african lyon?Mjanja huyu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad