Mwigulu Nchemba Awaonya Polisi Wanaowabambikiza Kesi Raia

Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba amewaambia askari wa jeshi la Polisi mkoani Katavi kufanya kazi kwa taratibu na sheria bila kumuonea mtu yeyote hasa wanyonge.

Waziri Mwigulu ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kutembelea makazi ya watanzania wapya pamoja na kuzungumza na askari wa jeshi la polisi, Magereza pamoja na Uhamiaji.

Mhe. Mwigulu amesema kuwa Askari hao waondokane na tabia ya matukio ya kuwabambikizia kesi raia kwa maslahi binafsi na kuwaonea na kusema kuwa serikali kali ya awamu ya tano haitamfumbia macho askari atakayebainika kufanya hivyo.

Aidha Waziri Mwigulu amechukua fursa hiyo kuwapa hamasa Askari hao kwa kusema kuwa serikali itawaboreshea maslahi yao kadri bajeti itakavyoruhusu ili waweze kufanya kazi kwa weledi zaidi.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Asante waziri tumechoka na kubambukiziwa kesi za uchochezi kila kukicha
    Mapolisi uchwara mmeyasikia haya toka kwa waziri ?
    Mwanasisa mwenzetu?

    ReplyDelete
  2. Mwigulu... Hongera hatutaki kumdhulumu mtu na wala asitudhulumu... Haki na sheria tuzifate sote katika majukumu yetu ya kula siku... tutazidisha mapenzi na undugu baina yetu na kujiona sisi ni wazalendo wa nchi hii na kila mmoja anawajibika katika nafasi yake kuleta maendeleo kwa nchi yetu na vuzazi vyetu na kuileta Tanzania mpya... chini ya mchapa kazi wetu baba JPJM... Hapa Kazi tu...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad