Mzee Yusuf Afanya Maamuzi Magumu

Gwiji wa mziki wa taarabu nchini Mzee Yusuf amethibitisha kuwa ameachana na kazi hiyo takribani miezi miwili iliyopita.

Taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii zimeeleza kuwa mwanamziki huyo ameachana na mziki na kuamua kumrudia Mungu.

Akizungumza na Mwananchi Digital kwa njia ya simu usiku huu, mmiliki huyo wa bendi ya Jahazi Modern Taarab amethibitisha kuwa taarifa hizo ni kweli na kuongeza:

“Nashangaa taarifa hizi zinasemwa leo. Ni suala la muda mrefu….takribani miezi miwili iliyopita na sababu ni kuwa nimeamua kumrudia Allah,”

Mwanamziki huyo mzaliwa wa Zanzibar alipoulizwa kuwa ni suala gani lililomsukuma hata achukue maamuzi hayo magumu, alijibu kwa kifupi, “ndivyo tunavyofundishwa na viongozi wa dini.”

Yusuph aliyetamba na vibwagizo kama “Nichumu, nikisi….mwaaaa,” katika baadhi ya nyimbo zake, amesema familia yake imeupokea uamuzi wake kwa mtazamo chanya na kwamba inamuunga mkono.

“Kwa sasa nitaimba kaswida zenye mafundisho ya dini,” amesema nyota huo huku akiahidi kufanya mkutano rasmi kuelezea suala hilo.

Mfalme huyo aliyeonekana kuwa ni gwiji wa taarabu ya kisasa (modern taarab) amezaliwa visiwani Zanzibar mwaka 1977. Aidha amejihusisha na sanaa nyingine kama maigizo.


Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hongera mzee yusuph kwa maamuzi yako. Allah akujalie na akuzidishie moyo wa kumcha na kumpwekesha. Ilala mtihani upo kwa ma Mrs je wako tayari kudumu katika stara?

    ReplyDelete
  2. Allah akusimamie kwa maamuzi yako mazuri

    ReplyDelete
  3. Alhamdelah Mwenyezi Mungu atuongoze na sisi muslimina wal musilimat hongera sana sana ni uamuzi mzuri

    ReplyDelete
  4. umeamua kumrudia mungu baada yakuchuma pesa haramu ambayo ndiyo utakayoitumia kuishi maisha baada yakuacha taarabu,acha kujidanganya wewe,sasa hizo mali na pesa ulizozipata kupitia mziki wa taarabu ambao ni haramu utazipeleka wapi na wewe umeamua kujitakasa kumrudia mungu wako??????nijibu

    ReplyDelete
    Replies
    1. USIMKATISHE MTU TAMAA .ALLAH NDIE ANAETOA MALIPO SIO WEWE.
      ULITAKA AENDELEE MPAKA AFE KWENYE HARAMU? CHUKI ACHENI

      Delete
  5. NAKUPONGEZA KAKA KWA UAMUZI HUO.MAANA HUJUI LINI UNARUDI KWA ALLAH.
    KWA VILE UNAKIPAJI CHA KUIMBA WAONAJE UKIIMBA NASHEED(NYIMBO ZA DINI

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad