Ama hakika kama siku haijafika haijafika tu.July 16 2016 nilimsindikiza binamu yangu kwa ajili ya matibabu nchini India,yeye alikuwa atangulie na ndege ya Oman Air kupitia Muscat mpaka India ambapo mimi ningefuata siku tisa au kumi baadae.Kwa bahati mbaya siku hiyo ilitokea "dhahama" uwanjani hapo na safari kuahilishwa,hivyo waliondoka siku inayofuata.
Mimi niliondoka tarehe 26 July 2016 na Fly Emirates kupitia Dubai(DXB) mpaka India,nakumbuka ndege hiyo kutoka Dsm ilikuwa flight #EK726 A6-EMW B777-300(Hii ndio ndege iliyoungua jana Dubai).Tuliondoka Dsm majira ya saa kumi na moja na madakika kuja Dubai.Hakika safari ilikuwa nzuri na tamu wakati wote.Nilifika India salama kwa kufanya "connection" Dubai mpaka Mji wa Hospital tuliyokusudiwa kumpeleka mgonjwa.
Mgonjwa wangu anasumbuliwa na pingiri za mgongo,kiasi amepata matatizo ya baadhi ya vidole na sehemu fulani fulani z mwili zisiwe na mawasiliano(nisizungumzie sana ugonjwa na mambo yake).Walipofika India,Walionana na "Specialist" tuliyopangiwa kuonana nae,ambae alimtazama mgonjwa wetu,hata baada ya matibabu,alishauri mgonjwa apelekwe kwenye tiba fulani ya asili huko huko India,ambayo inapatikana katika mji(?) wa Trivandrum,Kusini mwa India.
Kwa sababu jamaa ndio alielekeza huko,ghalama fulani za kwenda huko zikawa juu yake,as yeye tulishamlipa pesa nyingi tu kama "familia".Huko kuna tiba asili za hatari sana,na hakika mgonjwa wetu amepata nafuu na anaendelea na matibabu vizuri kabisa kabisa.
Kwa vile mie nilikuwa na kalikizo kama ka week mbili,ilinibidi nirudi mapema nyumbani,Tukaondoka siku ya Jumatano hapo Thiruvananthapuram, India(TVR) majira kama ya saa 0950(local Time) kupitia Dubai(DXB) ili nifanye connection ya kuja Dsm the same day.Unfortunately ndege niliyotoka nayo Dsm-DXB ile 26/07/2016 ndio hiyohiyo ilikuja TVR,hivyo ilikuwa Flight #EK521 A6-EMW B777-300.
Tulisafiri kwa raha mustarehe na mavyakula ya kihindi,full pilipili hadi kwenye hotsoup,ni safari ya zaidi ya masaa matatu na dakika kama 45 hadi 50.Njia nzima huko juu hakukuwa na tatizo lolote.Ni tabasamu za wahudumu wa ndege na mwendo wa movie na music mwanzo mwenga.Tulipokaribia kutuwa kama dakika kumi hivi,tukaambiwa tufunge mikanda na tuwe tayari kwa kutuwa,wale wenye "Air sickness" wakagawiwa kama tuvitambaa kujiziba macho ili wasibabaike na kizunguzungu wakati wa kutuwa.
Tukiwa tumeshaambiwa sasa "tupo tayari kutua" na ndio tumeingua DXB,ghafla tukaona tena ndege inarudi juu,yaani kama imetaka kutuwa halafu ikanyanyuka tena kwa kasi sana,baadae tukasikia sauti tu,tukae kwa amani,rubani ataenda kama feet4000 then tutarudi kutuwa kwa amani.Hata hivyo tukazungukaaa weeee,huku tunauona uwanja kwa pembeni...kama baada ya nusu saa hivi,tukaona wale wahudumu wanaanza kutuelekeza yalipo maboya(?) ya kujiokolea,na ule mlango wa emergency exit akahamishwa mtu akaletwa abiria mwingine,ambaye aliekezwa jinsi ya kuubandua ule na kupitisha wengine.
Baada ya hapo ikasikika sauti ya "emergency landing....May day May day"(kama nilisikia vizuri).Hapo ndio sasa matumbo jotooo...Lakini wahudumu hapo walizidi kusisitiza hali itakuwa shwari tusiogope maana hata watu wa uokoaji wapo tayari na kuna matatizo katika tairi za ndege ni kama zimegoma kutoka ili tutue...na tukaelekezwa kuwa milango itajifungua kama puto/pulizo,hivyo wakati wa kushuka ni kuserereka/sliding na sio kutembea....Haikuchukua muda tukajibamiza chini,ghafla moto mkubwa na moshi wa hatari...Mimi hata nilivyobebwa sijui nilibebwaje,nikajikuta eneo fulani zimejaa ambulance,polisi,madaktari na manesi tu...huku wengine waliopata mshituko wakiingizwa humo kwenda Hospital.
Kifupi wapo waliojikojolea(mimi nilijkuta nimelowa tu,sasa sijui nilijikojolea au jirani yangu alichafua).Kwa kweli nilikumbuka mpaka sala ya "Malaika Mlinzi" aliyonifundisha Mama nikiwa darasa la kwanza,niliona ujirani wa dunia na mbingu,uhai na kifo...hakika ndani ya saa nzima nilikuwa karibu na Mungu kuliko wakati wowote ule maishani.Wenzetu wanajiandaa sana,pale palikuwa na Sheikh na Mapadre(Wachungaji) kwa ajili ya kuombea ama waliotaka kufa au waliozidiwa..Mpaka nilijiuliza,hili tukio "lilipangwa" au wenzetu wana utayari sana wa matukio kama haya??
Baada ya hapo kila mtu alitazamwa afya yake,kupimwa pressure,sukari na kila kitu...na tukapelekwa hotelini,na jamaa wanasema asiondoke mtu kama anajisikia vibaya,tukae mpaka mtu anapoona afya yake ipo timamu..kwa kweli mimi sikuumia chochote zaidi ya mshituko na kuteguka "enka" wakati naserereka mlangoni,maana milangoni kulikuwa na kama maboya yale ya Watoto Kunduchi beach.Lakini nimepewa matibabu babu kubwa,na nipo hotel...wakaniuliza nahisi siku ngapi za kupumzika,nimewaambia siku 10 ntakuwa ok!!
Hapa nipo Hotel ya Five Star toka jana wakuu,nakula tu na kulala..kila baada ya muda anakuja Dr kunijulia hali,mpaka "najuta" kusema siku 10...ningeongezapo kidogo.Mizigo yetu imeunguwa,ikiwepo laptop yangu na simu mpya nilizonunua India Duty Free,jamaa wanasema wanatulipa kwa kilo na si kwa thamani ya vitu vilivyokuwemo.
Nawasalimu toka hapa DXB(Hotel kapuni maana nilitoroka kazini),nikiwa mzima wa afya,baada ya siku kumi nitarudi nyumbani na kwenda "kutambika" moja kwa moja kijijini kwa bibi.Nahitaji kutoa sadaka kubwa mbele za Muumba,kwa makubwa yaliyotokea.Hakika hautaji Mungu kuhamisha mlima toka sehemu moja kwenda nyingine ndio uamini ukuu wake.Ahimidiwe yeye aliyeumba mbingu na dunia
Daah pole sana,lakini ukiwa karibu na Mungu yatosha sana ndugu yangu,kama ulivyokuwa unamuomba katika hili,na
ReplyDeletehupashwi tena mambo ya matambiko kijijini kwa bibi bali shukrani na sadaka kwa Mungu tu basi.JINA LA BWANA LIHIMIDIWE,HALELUYA!
Pole kwa misuko suko ndugu yetu..Mungu amekusalimisha Roho yako nakuomba urehee kwake Na uwe kiumbe chema chenye kumuogopa Na kumtii. ..na uwe raia mwema mpenda Amani NA utulivyo Na kuchapa kazi..na mgonjwa wenu Allah atampa shiga Na kumuafu...karibu Sana nyumbani Na hakikisha kuwa geveva convention inatejelezwa kwa yalitokusibuni wote Na imani yetu kuwa wahusika wa shirika wanalifanyia kazi Na haki yenu mtapata ajili hawa wanatenfa haki Na kumuogopa mungu
ReplyDeleteMbona hizi ndege 2 hazifanani.moja ndodo nyinigine kubwa .pole
ReplyDeleteangalia wewe,wahanga wote wa ndege wana insurerance ,yaani wewe umetoka kimaisha subilia mamilion of dollars.mlipwe fidia..husiwe fala kaka km hujui fuatilia na lawyer ili mambo yaende kikanuni..inshaallah.
ReplyDelete