Ningelikuwa Magufuli Ningeruhusu Chadema Waandamane Kwa Amani Kuepuka Doa Kwa Serikali

Ningelikuwa Magufuli ningeliwaruhusu ‪#Chadema‬ wafanye maandamano na mikutano yao ambayo yako kisheria kwa mujibu wa katiba na sheria ya vyama vya siasa.

Kisiasa Chadema wameshinda, wana ajenda ambayo ina legitimacy ndani na nje ya nchi. Ajenda ni kuilinda na kuihifadhi Katiba. It is clear and simple to grasp kuwa MagufuliJP has somewhat thrown the law out of the window kwa kukataza mikutano na maandamano ambayo sheria ya vyama vya siasa imetaja kuwa ni halali. Kama Chadema watafanya walivyopania, any crackdown on them ni doa kubwa kwa Serikali ya Magufuli and a looser in the run ni ‪ CCM‬ kwa sababu Magufuli ni Mwenyekiti wa CCM

Ni wakati sasa CCM na Chadema warudi kwenye meza ya mazungumzo ‪Nchi‬ kwanza. Kwa nini CCM na Chadema ? @MagufuliJP ni Mwenyekiti wa CCM na makatazo haya yote yanainufaisha CCM si Serikali ambao kuilinda katiba ni jukumu lao.


Imeandikwa na Thomas David Maqway
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Enter your comment...Muheshimiwa Rais endelea kukaza uzi.huo muda wa kuandamana waende wakafanye kazi wajiongezee kipato pia taifa lisonge mbele.

    ReplyDelete
  2. nakuunga mkono.mimi pia nadhani wangepewa nafasi ya kuongea wangekuwa washamaliza pressure zao...tukaendelea kujenga nchi kwa kasi zaidi.saa hizi shughuli hazifanyiki vizuri...serikali,vyombo vya dola vime concentrate na UKUTA tu.Kimsingi mmeshawapa ushindi kabla hata ya maandamano maana message ishafika mbali duniani..everybody is asking what is UKUTA...UKIANGALIA SANA KUNA LOGIC...NCHI KWANZA..SHERIA NA KATIBA VIHESHIMIWE TUWARITHISHE WATOTO TAIFA LENYE MISINGI YA SHERIA...Jamani hatutaki fujo..tuna matatizo mengi ya kuhangaikia..hizi hela mnazotumia kwa issue ya ukuta ingesaidia hata matatizo ya maji ya vijiji kadhaa..BUSARA ITUMIKE.

    ReplyDelete
  3. Yetu macho
    Ila ziuumioza ni nyasi

    ReplyDelete
  4. Taifa linapoendeshwa kinguvu badala ya sheria matokeo ni haya. Ukawa wanalilia katiba ya nchi ili nchi iheshimike. Raisi hayupo huu ya sheria yoyote ya nchi. Raisi anachaguliwa na anaapishwa kupitia biblia au kurani kutegemea na dini yake kuilinda, kuitetea nchi, watu na mali za watanzania. Akiungana na polisi na vyombo vya usala kuhakikisha, kulinda mipaka, kuleta amani. Polisi hawanasheria yoyote kutangaza vita zidi ya watu wake. Wakuu wa mikoa na wilaya ambao wote ni wanachama wa CCM hakuna sheria yetote Tanzania inawapa uhuru kutangaza vita zidi ya wananchi. Na kukurupuka kutoa kibali kwa Raisi kuruhusu polisi na usalama juwinda watu , raia kama majangiri, au majambazi ni kupotosha nchi na ni kuleta machafumo nchini. Raisi kuzidi kukaa kimya ni wazi anashindwa kutengua alichokitangaza sababu kushindwa kutambua sheria zinazomwongoza namna gani afuate hizo sheria na si kujitungia zake.wakuu wa sini ambao mara nyingi maraisi anawatumia kuwasakia kura, kutangaza amani, wamekuwa waoga na kushindwa mufanya kazi zao kwa utashi na kumshauri Raisi na kumpa ukweli. Kuna viongozi wa dini akiwemo Gwajima bila woga almenena, na badala yake pia aNawindwa. Ni woga wa viongozi wengi ambao wanaogopa kukosolewa, kuambiwa ukweli na badala yake kutumia nguvu zido ya wananchi. Jeshi linapokwenda kati kati ya mji kujiandaa kivita zidi ya mwananchi asiye na silaha hii inaogopesha. Tuliona China , tanamen swuare, misri mabuldoza, Uganda, enzi za Amin, na vita ya kikabila Rwanda, Burundi, Sudan, lakini hata siku moja nilitegemea kuiona nchi yangu Tanzania kufikia hapa tulipofikia. Tumeona athari Zanzibar,na watanzania wanaokaa kimya kuilamu Ukawa, hawana uchungu na nchi yao. Watanzania wanaccm mnaokaa kimya na kutetea maslahi ya chama ambacho ni maslahi ya kikundi kidogo badala ya madlahi ya Taifa, hii ni ngumu kuielewa. Ilibidi raisi alopochaguliwa tu, kitu cha kwanza ambacho ilibidi akifanye ni kuhakiki amani Zanzibar, na kurudisha Katiba ya wananchi ambayo ingempa nguvu na kumsaidia sana kuiongoza, kuilinda nchi na watu na kutetea madlahi ya watanzania wote kwanza zidi ya wachache waliohujumu na wawekezaji waliokiuka miiko namna gani inabidi wafuate sheria za nchi hii katika uwekezaji. Badala yake wengi wametumia hongo, wamekuja kwa njia ya mazingira, environmental, na kujipa mali na utajiri kupitia viongozi wetu wa ngazi za juu bila kumhusisha Mtanzania toka ngazi za chini, viji, kata, wilaya, na mikoa. Watanzania wengi wamekuja kushtuka wameingiliwa bila mujua namna gani hawakujua. Ni hili linaloitikisa nchi yetu na Afrika nzima. Maligafi ya Afrika, uzembe wa viongozi wetu, uhaba wa elimu, uzalendo na woga. Nchi hii haitaendelea kwa washawasha, bakora, nguvu, mauaji, bali elimu, ushujaa, uchapaji kazi , umoja, amani ya kweli , upendo, utulivu, ujasiri wa kutambua na kujirekebisha pale tunapokosea. Turudishe Katiba, tutoe kinga kiinayomlinda kiongozi yeyote anayeruhusu mtanzania anyanyswe, abafhilike, Ibiwe, adanganye na asidanganywe, .inpe uhuru kila mtanzania kushiriki sawa, kuhiji, na kupata majibu yanayomtosheleza.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad