JESHI la Polisi, kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemnyima dhamana, Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya kumaliza kuhojiwa katika kituo kikuu cha polisi.
Baadhi ya viongozi waliofika kumwekea dhamana ni pamoja na Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema, Edward Lowassa Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa kamati kuu wa Chama hicho, aliyefika saa 12:14 jioni akiungana na viongozi na wanachama wa chama hicho.
Baada ya kufika Lowassa wanachama na wafuasi wa Chadema waliokuwa nje ya ofisi hizo za polisi walianza kuimba wimbo wa kumuita rais, rais, rais ikiwemo na kauli mbiu ya maarufu ya Peoles power.
Mara baada ya kufika alipokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe aliyekuwa amepanda gari moja na Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob waliokuwa nje ya geti.
Viongozi hao waliokuwa nje baada ya kuzuiwa kuingia ndani na polisi waliongozana na Lowassa kuomba kuingia lakini walizuiwa hali iliyofanya wachukue uamuzi wa kuondoka.
Kiongozi aliyeruhusiwa kuingia alikuwa ni Meya wa Dar es Salaam, Isaya Mwita.
Akizungumzia kuhusu hilo, Peter Kibatala mwanasheria wa Lissu alisema kwamba mahojiano kati ya jeshi hilo na mtuhumiwa yalianza saa 9:30 hadi saa 12:30.
“Katika maelezo ya polisi wanasema kwamba wakati Lissu akitoka mahakamani juzi kwenye kesi yake alitamka maneno ya uchochezi, lakini haya yote yanahitaji ushahidi,” alisema Kibatala.
Wakili huyo alisema kwamba polisi baada ya kumaliza mahojiano na wao wakiwa wameandaa utaratibu wa dhamana walikataliwa hadi leo Ijumaa atakapofikishwa mahakamani.
Polisi Wamnyima Tundu Lissu Dhamana, Atupwa Rumande
4
August 05, 2016
Tags
Huyu lissu Ni wa kutiea ndani Na kuhukumiwa bila dhamana kifungo cha muda mrefu Na kazi ngumu..ni mchovhezi Na muhatarishaji Amani ya nchi yetu akishirikia Na Na wachache wenye masilahi binafsi..hatukubali Na wala hatutowaachia wachache kuliongiza taiga letu la mamilioni katika majanga. Lissu Ni wa kifungo tuu Na kazi ngumu..siasa haijuu Na wala hatoijua Ni chuku Na tamaa Tu baada ya kukisa laivu Na posho..
ReplyDeleteHuwezi kumtukana rais wa nchi mbele ya hadhara kwamba ni dikteta uchwara. Huyu Lisu anataka afundishwe adabu kidogo
ReplyDeleteTena afundishwe adabu Na iwe Ni fundishi Na onto kwa wote walio Hai Na viumbe vilivyo HAI kwa ajili ea uhai Wao Na kuacha kutaguta Kiki kwa kukoda laivu..Hiyo jeuri ya kumtukana kikejeli mkuu haikubaliki Na hatuikibali Na wala usifikirie iko siku yatakunyamazia ..ukosefu WA nidhamu Kama juu Na ukisefu WA maadili kiasi hiki..unadhihirisha kuwa wewe Si mmoja WA jamii yetu Na sehemu yako maalumu iko Na wako tayari kukupokea Na kukuhudumia na kukufunza..kama Si serea basi labda isanga au kunakofanana Na huko..ajira pia NA kazi zipo pia..
ReplyDeletePosho inamtia wahaka Tundu mpaka anaanzisha Utundu..sema mlichoofanya Ni sawa Na muhakikushe huyu anapelekwa mahali pa saizi yake..Na Ajute kuufanya juu Utundu kamwe katila maisha yake..Mkuu WA nchi Ana Heshima Yake Na Nilazima sisi wananchi kumtii Na kutii sheria huwezi kutukana upendavyo mkosa nidhamu Na maadili...kiki za barabarani mwachie mdada wema Na siyo mtundu
ReplyDelete