Prof Lipumba:Sihusiki na Vurugu zilizotokea Katika Mkutano wa CUF

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Prof.Ibrahim Lipumba amesema hausiki na fujo wala vurugu zilizotokea ktk mkutano wa CUF na kuletea kusitishwa kwa mkutano huo.
Akijibu maswali kadhaa ya mwandishi wa Habari wa Azam Tv,Prof.Lipumba anasema ni kweli yeye kama mwenyekiti aliyejiudhuru hakualikwa wala hana vigezo vya kuingia ktk mkutano huo,lkn akiwa nyumbani alipata ujumbe wa simu ya mkononi kuwa anahitajika ukumbini na baadhi ya wanachama wanataka arudi katk nafasi yake.

Baada ya kupata ujumbe huo,Lipumba aliamua kuondoka nyumbani kwake na kwenda ukumbini,ambapo kimsingi kikatiba na kikanuni hakuwa na ruhusa ya kuingia,lkn kwa nafasi yake ktk chama alipaswa kuruhusiwa kuingia japo walinzi walimgomea wakisema haitajiki kwa muda huo,yeye alilazimika kuhakikisha anaingia ili kuweza kukidhi kiu ya wanachama waliomhitaji na wanaoona anafaa kurudia nafasi yake.

Prof Lipumba anasema hakuna mwana-CUF anayeijuwa CUF kama yeye na wala hakuna mwana-CUF toka Tz bara na hata visiwani ukitoa Maalim Seif aliyeweza kuwatetea Wazanzibar kama yeye,akitolea mfano wa kudai haki ya mwaka 2001 na harakati nyingine za kuwasemea na kuwatetea Wazanzibar.Lipumba anasema yeye ndiye kiongozi aliyezunguka Tz bara na visiwani na kufahamiana na viongozi wa ngazi zote na ndio hao wanaomtaka arudi ktk nafasi yake.

Akijibu swali la kuwa "anatumiwa na Watu kuivuruga CUF"...Prof Lipumba anasema hawezi kuihujumu CUF kwa sabbu yeye ndio sehemu ya waasisi wa chama hicho na amekipigania kwa miaka mingi ndani ya jasho na damu,hivyo kuwataka viongozi wa CUF Taifa kutumia hekima na kuacha maamuzi ya wanachama wanaotaka yeye arudi na kuchukuwa nafasi yake na kuendeleza harakati za kuindoa CCM madarakani kuelekea 2020.

Prof anasema bado ana imani kuwa wanachama wanataka yeye arudi na ndio maana hata baada ya kuwa yeye si sehemu ya mkutano kikatiba na kikanuni,bado kuna wanachama walimpigia simu afike ukumbini na kujuwa hatima yake ya kurudia nafasi yake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad