Sababu za TAKUKURU Kumkamata Rais wa Simba Evans Aveva

Asubuhi ya August 4 2016 taarifa zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na Rais wa Simba Evans Aveva kutiwa mikononi mwa Polisi kutokana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kuagizwa kukamatwa kwa kiongozi huyo. millardayo.com ilifanikiwa kumpata kaimu afisa msemaji wa TAKUKURU Tunu Mleli na kuweka wazi.

“Ni kweli Aveva amekamatwa na polisi baada ya TAKUKURU kuagiza hivyo kutokana na tuhuma za rushwa zinazomkabili, tuhuma zinazomkabili ni uchepushwaji wa fedha kutoka account ya Simba kwenda katika account yake na baadae kuanza kufanyiwa mgawanyo katika account nyingine, ni fedha za usajili wa Okwi kutoka Etoile du Sahel”
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Daah,Aveva utadhani hana shule jamani,hapo mengi yatachokonolewa na hata ile ripoti ya mapato na matumizi yanatakiwa kuuangaliwa na
    ndio maana kulikuwa na kigugumizi kuuza timu kutoka kwa uongozi wa simba.

    ReplyDelete
  2. USHAMBA TU,INA MAANA HAKUJUA KAMA DUNIA YA SASA IKO KIGANJANI?
    HAYA SUBIRINI MBATIZWE KWA MOTO.HAPA KAZI TU!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahhahahahah,mbona kubatizwa kwa moto.

      Delete
  3. Huyu jamaa na wenzake wanataka milion 130 kwa ajili ya Kessy,naamini lengo ni kumkomoa tu asicheze kijana wa watu,na wakumbuke ni sawa na mtoto wao na amewatumikia klabu yao,na hata kama kakosa sio kumtafutia adhabu kubwa ya hivyo.Sasa hizo mil.130 na zenyewe zingefanywa hivyohivyo.Binadamu tuache roho mbaya.Sio shabiki wa SIMBA/YANGA lakini inaumiza kijana mdogo kama Kessy apoteze kipaji chake.Mungu hapendi na malipo ni hapa hapa duniani.Pole yake lakini TUJIFUNZE.

    ReplyDelete
  4. uwii kwa sasa ndio habari ya mujini

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad