Watu wanaoaminika kuwa ni majambazi usiku huu wamevamia Benki ya CRDB iliyopo Mbande wilayani Temeke mjini hapa na kuua askari kisha kupora silaha na kutokomea kusikojulikana.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alipoulizwa kuhusu tukio hilo, amesema hawezi kuzungumza chochote kwa maelezo kuwa yuko eneo la tukio na amesema atafutwe kesho.
Uhalifu huo umetokea ikiwa umepita mwaka mmoja tangu kutokea kwa tukio la majambazi kuua askari wanne na kupora silaha baada ya kuvamia kituo cha Polisi Stakishari, Ukonga jijini hapa.
Sirro nawe ni jipu
ReplyDeleteUlikuwa busy kunadi fulana za ukuta
Badala ya kuwa busy kuangalia hali ya usalama ya jiji
Hufai itumbuliwe uko busy sana na media kila kukicha