Tundu Lissu Funga Kazi, Polisi Watweta

TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki amefikishwa katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam kwa mahojiano, polisi wamekuwa na kazi ya ziada, anaandika Shaban Matutu.

Idadi ya polisi kwenye kituo hicho imeongezwa wakati alipofikishwa huku shughuli nyingine ndani ya kituo hicho zikionekana kusimama.

Awali, Lissu ambaye ni Mwanasheria wa Chadema hakua akijulikana alipo kutokana na polisi kutotoa taarifa kamili baada ya kumkamata jana jioni.

Lissu amefikishwa kwenye kituo hicho leo saa 7:54 mchana na gari aina ya Land Cruser lenye namba za usajili T 312 CWM akiwa chini ya ulinzi mkali.

Amefikishwa kwenye kituo hicho kwa ajili ya mahojiano kutokana na madai ya kutoa kauli ya kichochezi ‘dikteta uchwara’ juzi wakati akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipoenda kusikiliza kesi ya uchochezi iliyohusu kauli yake ya awali ya ‘dikteta uchwara’.

Wakati Lissu akifikishwa eneo la kituo hicho, polisi walikuwa wamezunguka eneo hilo huku kukiwa na  ulinzi mkali pamoja na silaha za moto.

Askari waliokuwa eneo hilo walikuwa wakiwaondoa wananchi na waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia matukio katika eneo hilo.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa alifika kituoni hapo saa kumi kasoro, hata hivyo alizuiwa kuingia ndani.

Saa 4:02 Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam kituoni hapo na gari lenye namba za usajili SM 10584 ambapo aliruhusiwa kuingia ndani kumuona Lissu ambaye anahojiwa.
Lissu bado anaendelea hojiwa…
Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na nyie udaku ni jipu eti lisu funga kazi mbona ktk habari hukuthibisha kafunga vipi kazi mnapenda kukuza habari bila mpango

    ReplyDelete
  2. Huyu Ni wa kutiea ndani Na mahakama haraka iwezekanavyi bila ya dhamana kwa kumtolra kashifa Na lugha chafu mkuu WA nchi Na bila ya uyeyezi manake tumeyasikia laivu..kiki wanazozitaka hazina mshiko Na wala Hana haki ya kutoa maneno Na kuita majina ya kashfa kwa kiongozi wetu baba JPJM..ni mchovhezi Na meanasheria wa serikali amfungulir jalada lingine la kesi Na kifungo cha muda mttefu..mashahidi tupo Na ushahiddi tosha upo..siasa haziwezi Na pia hazijui Na inadhihirisha chuku tuu

    ReplyDelete
  3. Tanzania imekuwa hivi
    Jamani
    Yetu macho lakini sitoshangaa
    Kuona vita inakuja si muda mrefu

    ReplyDelete
  4. SASA KWANINI MMESEMA TUNDU LISU FUNGA KAZI? FUNGAKAZI KWA KUKAMATWA AU? ACHA MBWEMBWE. KUWENI WAZALENDO

    ReplyDelete
  5. Polisi wa Tanzania ni polisi UCHWARA
    U make us sick
    Neno uchwara mlivalie njunga
    Papa the most powerfully in the world
    Queen Elizabeth , Obama
    Hizo ni lugha za kisiasa
    Msilazimishe watanzania wapende mnachokitaka
    Hata Nyerere tulimwita Mchonga kwa ajili ya meno yake
    Mkapa fuso kwa uso wake

    ReplyDelete
  6. VIVA Lissu, ViVA CHADEAMA, VIVA Singida, VIVA Wanamageuzi wote-aluta continua

    ReplyDelete
    Replies
    1. Samora Michael alikiea Kongwa Na MPWAPWA..DODOMA..Msumbiji imeshapata Uhuru

      Delete
    2. Tundu Ni mkosefu WA Nnidhamu Na maadili..hili Si geni tumemuona katila Bunge ..na Ni mmoja WA eapenda sifa bila Kisi Na kuondoa Bunge laivu kumemkoroga Sana kwa hiyo ameamua kuanzisha sokomoko mtaami lakini Ni baada ya kubugi stepu..utanyea debe kwa muda mrefu mkoda nidhamu wewe utakuja kuiona Tanzania mwaka 2040 Kama iko hai hapo wewe Si mbumge WA haiii

      Delete
    3. Frelimo R.I.P SAMORA..UANAHARAKATI BAADA YA UKOMBOZI NA UHURU..UMESITISHWA NATURALI

      Delete
  7. Sio dikteta uchwara,ni lidikiteta lichwarachwara yani halina mbele wala nyuma

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad