Utafiti: Watz Wengi Wameajiriwa Kwenye Ulinzi

Wanzania haiwezi kupiga hatua kimaendeleo na kupunguza tofauti ya hali ya maisha na kipato kwa watu wake iwapo idadi kubwa ya nguvu kazi ipo kwenye sekta ambazo hazina umuhimu mkubwa katika uzalishaji.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya Society for International Development - SID ya nchini Canada na yenye ofisi zake jijini Nairobi nchini Kenya Bw. Arthur Muliro, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa ripoti ya hali ya kipato kwa wakazi wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki, ripoti iliyotolewa jijini Dar es Salaam hii leo.

Katika maelezo yake, Bw. Muliro amesema utafiti umeonyesha kwamba zaidi ya Watanzania milioni moja wameajiriwa kwenye sekta ya ulinzi na masuala ya usalama, idadi aliyodai kuwa ni tofauti na katika sekta nyingine muhimu kama za uhandisi na wataalamu ambao kwenye baadhi ya sekta idadi yao haizidi watu elfu kumi na sita.

Ameshauri kuwa juhudi kubwa zinahitajika kuongeza wataalamu kwenye sekta zilizoajiri watu wengi kama kilimo ambacho takribani asilimia themanini ya watanzania ndiyo wanayoitegemea kwa ajili ya kuendesha maisha yao.

Ripoti hiyo imetolewa na taasisi inalojihusisha na uboreshaji mazingira ya biashara, uchumi na uwekezaji kwa nchi za Afrika Mashariki ya Trade Mark East Africa ambapo SID ndiyo iliyofadhili utafiti huo uliohusisha nchi za Tanzania, Uganda, Rwanda, Kenya na Burundi.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Uchochezi mwingi
    Lazima na walinzi wengi

    ReplyDelete
  2. wengi hawawezi kutumia akili wamejaliwa kutumia nguvu,. wanakimbilia sekta za kibabe na kiongozi wao mbabe.

    ReplyDelete
  3. Maneno yako mwenyewe yanaonyesha were no mbabe ndani yamawazo yako we we emotioni huna mawazo ya ziada utaishia kulamu badala ya kujenga hujui kuwa ridhiki ya MTU hupangwa na mungu...tumia akili katika kuchangia mada...

    ReplyDelete
  4. Binadam wengine hawajitambui...sijui hata familia zao wanaziongoza vipi.
    Arejee mada inavyosema,uko sawa kiongozi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad