Waraka wa Wazi Kwa Rais Magufuli Toka Kwa Mbunge Godbless Lema "Haki Huinua Taifa"

Mh Rais nakusalimu, sasa ni usiku wa manane nimeamka nikiwa natafakari mambo mengi lakini zaidi sana ni kuhusu mwenendo wa demokrasia katika Nchi yetu, nimekosa usingizi kabisa nikifikiri ni namna gani ninaweza kusaidia kwa mawazo yangu kufanikisha nia yako njema katika ustawi wa Nchi yetu.

Mheshimiwa Rais na kabla sijaanza kuandika waraka huu kwako, nimesali nipate hekima ya kutosha juu ya maandishi haya ninayoandika na wewe pia nimekuombea sana kwa Mungu, kwani baada ya mimi na Wabunge wenzangu kufukuzwa Bungeni kwa kudai matangazo ya Bunge live nilikwenda kijijini kwetu kusalimia wazazi wangu, na nilipokuwa nawaelezea kwanini nimefukuzwa Bungeni matamshi yangu yalikuwa na laumu nyingi dhidi ya Serikali yako, Mama yangu aliniuliza kama huwa nakuombea kwa Mungu kama Rais wa Nchi, sikuwa na jibu la uaminifu kwake na hivi ndivyo alivyoniambia “ KAZI YA URAIS NI NGUMU, KILA MARA UNAPOSALI USIACHE KUMWOMBEA RAIS WA NCHI, MUNGU AMAJILIE AFYA NJEMA, HEKIMA NA BUSARA KWANI RAIS AKIKOSEA KUAMUA NI NCHI IMEKOSEA SAFARI YAKE YA MAFANIKIO NA USTAWI, KWA HIYO MUOMBEE RAIS SIKU ZOTE “

Mheshimiwa Rais, ulikuwa ni husia muhimu sana kwangu lakini mgumu sana kwa wakati huo, lakini baada ya kutafakari, kuanzia siku hiyo mimi na Familia yangu tumekuwa tukikuombea sana kwa Mwenyezi Mungu ili Nchi yetu isikosee safari yake ya mafanikio yaliyojaa Ustawi bora na Uhuru.
Mheshimiwa Rais, kama ambavyo naamini Watu wengi wanakuombea na Sisi pia tunaomba utuombee, Mungu atujalie hekima, busara na uvumulivu juu ya maumivu tunayopitia wakati tunapojaribu kutekeleza wajibu wetu wa kidemokrasia katika Nchi yenye msingi wa demokrasia lakini kwa bahati mbaya sana kazi zetu za siasa zimekuwa ngumu sana na mashaka kuliko hata wakati ule wa ukoloni.

Mheshimiwa Rais, Ukimchukua ndege porini ukamfuga nyumbani ,ukamtengenezea kiota cha pamba na sufi, ukampa chakula chake kwa ufasaha na asikose maji ya kunywa tena masafi ya chupa ya Kilimanjaro, ukamfungia ndani asipate tabu juani, hakika siku ukiacha mlango au dirisha wazi ataondoka na hatarudi, atakwenda porini akatafute asili yake na Uhuru wake, atakwenda kutafuta chakula kwa shida, maji kwa shida, lakini lengo muhimu ambalo ni Uhuru litampa faraja kubwa ya kwamba ameondoka kizuizini.

Mheshimiwa Rais, unaweza ukatupa chakula, elimu, afya, na mambo mengi muhimu, lakini ukitunyima Uhuru wa kusema, tukaishi kwa hofu kama tuliyonayo sasa, Mheshimiwa Rais nakuhakikishia siku ukiacha dirisha wazi tutatoroka na kamwe hatutarudi. Aliyekuwa Rais wa Libya Hayati Muhamar Gaddafi, alifanya kazi kubwa ya kujenga Libya hata mahari watu walilipiwa na Serikali walipotaka kuoa, watu walipewa nyumba na mambo mengi muhimu, lakini Gaddafi alisahau kuwa hakuna zawadi kubwa kwa Binadamu zaidi ya Uhuru.

Mheshimiwa Rais, ruhusu Watu waseme, acha Watu wapige kelele, ruhusu mioyo yao ipumue, wacha Watu wakosoe jambo hili halitakuwa balaa kwako bali Baraka. Kama kweli unayo nia njema, njia pekee na muhimu tu unayoweza kuthibitisha nayo nia yako njema ni kuruhusu mfumo wa demokrasia wa Vyama vingi kukua, umekuwa ukipigana sana na mambo mengi machafu yaliofanywa na Serikali ya Chama chako huko nyuma, umethibitisha kwetu kwa kiwango fulani na kwa umma wote hali mbaya uliyoikuta Serikalini baada ya kuingia Ikulu, hili funzo tosha kwako kwamba namna pekee ya kusaidia Taifa hili ni kujenga demokrasia ya dhati na kufufua matumaini ya Watanzania kwa kuwapa Katiba bora waliyoitaka, ambayo hata kama uwepo wako hautakuwepo Watanzania watakuwa salama na watasonga mbele.

Mheshimiwa Rais, mamlaka uliyonayo yanatokana na Katiba , Wewe ni Kiongozi Mkuu wa Nchi kwa sababu ya Katiba, Majeshi yote yanakutii wewe ni kwa sababu ya Katiba, uteuzi wote unaofanya wa Viongozi katika utawala na unaowatumbua, mamlaka hayo pia umepewa na Katiba, mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa pia ni matakwa ya Katiba na tumepewa na Katiba ,na wote sisi kwa dini zetu mbali mbali na makabila yetu wote tunakutana na kuunganishwa na Katiba na kuheshimu Katiba kama msingi mkuu wa uendeshaji wa Nchi.

Mheshimiwa Rais, Mungu adhihakiwi kwani apandacho Mtu ndicho avunacho,Wazazi wengi wanalia sana siku hizi juu ya tabia ya kwamba watoto wao wamekuwa walevi na wenye adabu mbaya, lakini ukifanya utafiti karibu nyumba zote za kisasa zinazojengwa siku hizi ramani ya nyumba hizo hazikosi baa ndogo ndani ya nyumba hizo, kama hatuwezi kufanya tunayo ruhusiwa na Katiba na anayetuzuia kufanya hivyo mamlaka yake yanatokana na Katiba, hakika mbegu inayopandwa hapa ni hatari kwa ustawi wa Taifa, iko siku amri ya utekelezaji juu ya masuala muhimu haitachukuliwa kwa sababu umuhimu wa kuheshimu Katiba na utawala wa sheria hautakuwepo.

Mheshimiwa Rais, Haki huinua Taifa,tuanapoelekea tarehe 1/09/2016, CHADEMA imeitisha mikutano ya hadhara kote Nchini pamoja na maandamano, tayari kauli yako na viongozi wengine wa juu wa Serikali wameonya juu ya Mikutano hiyo na kusema hatua kali zitachukuliwa bila huruma dhidi ya watu wote watakaojitokeza kuunga mkono harakati hizo.

Mheshimiwa Rais, tunafahamu Jeshi la Polisi liko imara kupambana na kuzuia haki hii ya Kikatiba, pengine Watu wataumia na wengine watakufa, je ni kweli tunahitaji kufika huko? je hatuoni kuwa matakwa ya Katiba yakizingatiwa risasi wala bomu havitatumika, maandamano haya yameitishwa kushinikiza haki yetu ya Kikatiba ya kufanya mikutano, Uhuru huu wa Katiba ukizingatiwa kwa kuruhusu mikutano ya hadhara hakika ni kwamba maandamano hayatakuwepo na kusema kwamba Sasa ni Kazi tu, na mikutano yote ya Siasa isubiri 2020, je ni halali Mkristo kusali siku ya Noeli (Christmas ) tu ? au Mwislamu kuingia Msikitini siku ya Idd tu?

Mheshimiwa Rais, Siasa ni Kazi na ndio maana wewe ni Rais kwa sababu ya Siasa na Mimi ni Mbunge kwa sababu ya Siasa, tena ni kazi muhimu sana tu kwani ndio mfumo pekee unaotafuta utawala wa ngazi mbali mbali na wa juu kabisa katika Nchi.

Mheshimiwa Rais, lakini pia kufuatia kauli yako ya kwamba kila Mtu afanye mkutano kule alikochaguliwa ni hatari kwa ustawi wa Taifa letu na mshikamano kwani tunajenga siasa za ukanda na ukabila katika Nchi yetu. Mkoa wa Kilimanjaro ccm ina majimbo mawili tu, maana yake CCM hawatakiwi kufanya mikutano ya hadhara na siasa sehemu nyingine za Mkoa wa Kilimanjaro? Mkoa wa Geita hauna hata Jimbo moja la Upinzani, je huko nako vyama vyetu havitakiwi kwenda kufanya mikutano na ujenzi wa chama? Je, ikiendelea hivi huoni kuwa tutaanza kujenga misingi ya kugombania nafasi za siasa kule ambako ni asili za makabila yetu tu?

Mheshimiwa Rais, jambo hili litaleta mpasuko katika Taifa letu ni kauli inayopaswa kerekebishwa haraka , hivi Karibuni Msemaji wa ccm Ole Sendeka alifanya Mkutano Longido, je Ole Sendeka ni Mbunge wa Longido? au Polisi wa Mkoa wa Arusha hawakusikia tamko lako?

Mheshimiwa Rais, nakuomba sana utambue kwamba, unyenyekevu sio utumwa wala uzembe, ukizingatia matakwa ya Katiba hakuna mwenye hekima hatakaye kudharau, wewe ni Binadamu unaweza ukufanya makosa usiruhusu mikono yako ikashika damu pasipo sababu ya msingi ni laana kwa Taifa na Kizazi chako.

Mheshimiwa Rais, na kama jambo hili ambalo liko wazi katika Katiba yetu halitaweza kupata fikra yako na mwelekeo mpya wa mawazo yako, basi itakuwa ni dhahiri kwamba unachokitafuta katika utawala wako sio haki ya Watanzania bali ni utukufu binafsi. Na suala lolote kuhusu utukufu ni suala linalomuhusu Mungu na sio Binadamu

Mheshimiwa Rais, Polisi wanajiandaa kwa sababu ni muhimu wakatii amri ya Amiri Jeshi Mkuu, wasipofanya hivyo watakuwa wanafanya uhaini, lakini ni vyema ikajulikana kwamba, dhamira ikichoka huwa inatamani mauti, tukikaa kimya huku dhamira zetu zikiumia ni hatari kuliko kupiga kelele kwa sauti kuu, ni maombi yangu kwa Mungu kwamba muufaka wa utata huu wa Uhuru wa Vyama vya Siasa unaotokana na Katiba uwe umepatikana mapema iwezekanavyo ili kuepusha hatari inayoweza kutokea na kusabibisha maumivu , hasara, vifo na utengano katika Taifa letu.

Mheshimiwa Rais, wakati Polisi wanajiandaa kukabiliana na waandamanaji wanaodai haki yao ya kweli, chuki kubwa inaendelea kujengwa kati ya walinzi hawa wa amani na raia, mashaka yangu ni kwamba kunaweza kutatokea mpasuko mkubwa huko mbele ya safari kati ya Polisi na raia, maisha ya visasi yataanza mitaani na mwelekeo mbaya wa Taifa letu unaweza kutokea.

Mwisho, Mheshimiwa Rais, nakutakia kila la kheri na Mungu akubariki sana katika kazi zako na maamuzi yako ya kila siku , ila siku zote kumbuka" Haki huinua Taifa"

Never forget that justice is what love looks like in public“ Cornel West
“injustice anywhere is a threat to justice everywhere” Martin Luther JR“
“Peace and justice are two sides of the same coin“ Dwight D.Eisenhower
“All the great things are simple , and many can be expressed in a single word, freedom , justice, honor, duty, mercy, hope” Winston Churchill
Godbless J Lema (MB)

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ukweli mtu mh raisi waache wanasiasa wafanye kazi Yao, mbona unaogopa tatizo lipo wapi

    ReplyDelete
  2. God less Wema, Umejitahidi kutua ndikia na umejitahi kujiweka katika uelewa na Kazi ngumu na mzuri inayofanya na Mh Raisi wetu JPJM katika awamu hii ya yetu ya Tano Yenye nia na Lengo la kumtumikia Mtanzania na Ukiwemo wewe God less. Mia kama kawaida yako au yenu umeleta sera ya kujidhihirisha kwamba wewe hivi sasa uko katika kukosa usingizi je unajua ni kwa ajili ya nini? na kujionesha kuwa wewe ni katika wale wenye kuiona demoklasia inabanwa au inafinywa.. Ndugu zangu wazalendo kama we na wanavioja wenzako ambao tumeamua kuwapumzisheni na sokokomoko zenu katika bunge letu ili msiendelee na upoposhaji na ukosefu wa nidhamu uliokidhiri na mpaka tukikutana nje mnaulizana mpya gani unaleta leo.. Hii ndiyo hadi mliyofikia na kutokuwe laivu ikawachanganya zaidi na posho ndiyo ikakukaribisheni Mirembe.. Lema wewe ni kijana mdogo unahitaji kuiangalia familia yako na ndugu zako na wana kata na kitongoji chako na mengine ambayo kwa sasa bado yamefunikwa yanayo kuhusu wewe katika maisha yako ambayo mwisho wake unapajua yaache yasitirike,, Tafuta ajira ya zaisi yako ili uendelee kuchangia katika ujenzi wa taifa kuleta maendeleo na sio Siasa na maneno ya kubuni kaman DENCLACHIA / BANANALASI / SHASI/ NA MENGINE MENGI AMBAYO UKIULIZWA TAFSIRI YAKE INAKUSHINDA... KUMBUKA MOJA... HAPA NI KAZI TUU..

    ReplyDelete
  3. God less Wema, Umejitahidi kutua ndikia na umejitahi kujiweka katika uelewa na Kazi ngumu na mzuri inayofanya na Mh Raisi wetu JPJM katika awamu hii ya yetu ya Tano Yenye nia na Lengo la kumtumikia Mtanzania na Ukiwemo wewe God less. Mia kama kawaida yako au yenu umeleta sera ya kujidhihirisha kwamba wewe hivi sasa uko katika kukosa usingizi je unajua ni kwa ajili ya nini? na kujionesha kuwa wewe ni katika wale wenye kuiona demoklasia inabanwa au inafinywa.. Ndugu zangu wazalendo kama we na wanavioja wenzako ambao tumeamua kuwapumzisheni na sokokomoko zenu katika bunge letu ili msiendelee na upoposhaji na ukosefu wa nidhamu uliokidhiri na mpaka tukikutana nje mnaulizana mpya gani unaleta leo.. Hii ndiyo hadi mliyofikia na kutokuwe laivu ikawachanganya zaidi na posho ndiyo ikakukaribisheni Mirembe.. Lema wewe ni kijana mdogo unahitaji kuiangalia familia yako na ndugu zako na wana kata na kitongoji chako na mengine ambayo kwa sasa bado yamefunikwa yanayo kuhusu wewe katika maisha yako ambayo mwisho wake unapajua yaache yasitirike,, Tafuta ajira ya zaisi yako ili uendelee kuchangia katika ujenzi wa taifa kuleta maendeleo na sio Siasa na maneno ya kubuni kaman DENCLACHIA / BANANALASI / SHASI/ NA MENGINE MENGI AMBAYO UKIULIZWA TAFSIRI YAKE INAKUSHINDA... KUMBUKA MOJA... HAPA NI KAZI TUU..

    ReplyDelete
  4. TAARABU?KHAA!HAPA KAZI TU!

    ReplyDelete
  5. BADO KIDOGO MTAMKUBALI TU MAGUFULI,NA MUNGU WETU AZIDI KUMPA ULINZI TUKIAMINI DUA ZETU ANAZISIKIA.

    ReplyDelete
  6. SHUT UP LEMA.

    ReplyDelete
  7. Kwendraaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  8. Nampongeza Sana Mhe Lema. Rais sio Mungu na ole Wenu Mnaompa Utukufu Rais Mkisahau Kuwa NAYE ni binaadamu kama nyie.

    Nchi ina KATIBA na SHERIA zake Ambazo zinatuongoza watanzania wote na ndizo zinazotakiwa kumwongoza Rais wetu katika maamuzi yake.Kauli za Rais sio SHERIA wala KATIBA, ole wenu mnaogeuza na kuzilinda kauli za RAIS kuwa SHERIA kwa kisingizio cha "HAPA KAZI TU".

    Miaka 54 TOKA UHURU mlikuwa wapi?? Ina maana Hamkujua kufanya KAZI?? Hizi Kauli Mbiu za Kuvuma na Upepo Inatupasa Tufahamu huku ni KUDANGANYANA. Mfumo mbovu uliopo nani alaumiwe CHADEMA au CCM ??.

    Nikauli mbiu ngapi za kuvutia zimetufikisha kwenye umaskini na ujinga ?? . UKIWA KAMA MTANZANIA UNATAKIWA UFAHAMU KUWA SIASA SIO DAWA YA MATATIZO YENU.

    Watanzania wengi wanaamini Mhe RaisMagufuli sio mwanasiasa ila FAHAMU kuwa katika MARAIS WANAOJUA KUCHEZA NA SIASA za NDANI KATIKA BARA LA AFRIKA KATIKA KIWANGO CHA JUU CHA UELEWA MHE. RAIS MAGUFULI ANAWEZA KUSHIKA NAMBA MOJA AU MBILI! MFUMO ANAOTUMIA KUTAWALA UNAITWA " AUTHORITARIANISM " .
    PEKUA GOOGLE NA VITABUNI USOME MFUMO HUO ILI UFAHAMU KWA NINI MHE LEMA AMEANDIKA HIYO BARUA YA WAZI KWA RAIS WETU MTUKUFU.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Chato umetafakari vyema. Mhe. Lema umeandika maneno yenye mantiki kubwa, lakini pole sana, kwa kuwa NI KAWAIDA YA MTANZANIA KUJIONA ANAJUA KILA KITU HATA KAMA SHULE HAKWENDA AU ALIFELI. MH. LEMA TUSAMEHE WATANZANI WENZAKO, SIO KOSA LETU, NA PIA NAJUA UNAFAHAMU, LAKINI UMEANDIKA MAMBO YENYE BUSARA KWA WALIOELIMIKA.

      Delete
  9. Wewe mdau uliyeandika unamjua Godless au umemsikia kwenye ile miaka ya laivu? Sasa kwa taarifa yako ita majina upendavyo na Kama. ulieleweshwa au ilitafsiriwa maana ya authoritarianism na mataifa ambayo Leo yameendelea na yamekuwa makubwa hii ndiyo nilikuwa serial I onavyofanya na wapiga filimbi nyingi Kama hakuozea jela Bado walipigwa hizi ya ajili na filimbi haikuwa na upepo tena na ucheleweahaji wa maendeleo haukuwepo kwa hiyo kuwa mzalendo tufanye kazi kwa ufaniai na tafuta ajira ambayo utakuwa mzalishaji kwa manufaa ya faida vinginevyo pumzika waache wanaume was hike jembe.. unataka uwanja wa Sera kumbuka utakuja na nafasi utapewa huko 2040 he kwa sasa Una umuri gani???

    ReplyDelete
  10. fuyhuiohu gyggt gygtf 564

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad