Wasanii Wapenda Amani Waungana Kupinga Maandamano UKUTA Ya Chadema

WASANII mbalimbali wanaopenda amani wameungana kwa pamoja kupinga maandamano ya UKUTA yanayotarajiwa kufanyika Septemba Mosi, mwaka huu.

Akizungumza jana mbele ya Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Wasanii hao wapenda amani, Steve Nyerere alisema hamna haja ya maandamano bali tunahaja ya kufanya kazi hususan kwa vijana.

"Vijana ndio muhimili mkubwa kulinda amani ya nchi,tusiwaze maandamano bali tuwaze je Akinamama na Watoto wanapata huduma hospitali"alihoji Steve Nyerere.

Kwa Upande wa Makamu Mwenyekiti wa Wasanii hao, Asha Baraka alisema wameamua kupaza sauti zao kwa niaba ya Wasanii wote wanaopenda amani.

Alisema Tanzania ni nchi ya Amani sio nchi ya vita hivyo wanapofanya shughuli za UKUTA shughuli zote za kijamii zitasimama.

Hatahivyo aliomba Septemba 1,  UKUTA wasimamishe maandamano hayo, pia watafute njia muafaka ya kuweza kuongea Vyama kwa Vyama na wakapata muafaka ili nchi iweze kwenda mbele.

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hamna lenu jambo
    Subirini bado kuna vyeo kibao mtapata
    Otherwise subirini 2020 mtupigie kampeni
    Mungu awabariki

    ReplyDelete
  2. ukuta mbele wa mbeleeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  3. Wataandamana watoto wa wajinga wasio na kazi za kufanya, hivi mtu unashughuli zako, anawezaje kukuandamisha mtu siku ya Alhamisi!! Kweli wajinga ndio waliwao.....huyo muandaaji mkuu wa hayo maandamano anajiandaa kusafiri.....tunaomba wanausalama muhakikishe hakuna kiongozi yoyote wachadema anasafiri, wote wawe mbele waongoze maandamano........... ticket ya Mbowe Freeman imevuja akijiandaa kusafiri na Emirates tarehe 1/9, hakikisheni HAONDOKI, nayeye lazima aonje JOTO-YA-JIWE.......asituletee zake za MKONO-KU-UGALI-MACHO-KU-MCHUZI yake hapa, yote yatakaa sawa siku hiyo....mfyuuuuu


    ReplyDelete
  4. uyo styve nyerere aelewi na grup yake wanacho kiongea. kasema nani kama ukuta ni vita. Tz yetu wote. kila bin adam anamapungufu yake. Tanzania mbele vyama baadae

    ReplyDelete
  5. Ningefaaaass kuwa mkuu wa wilaya kinondoni
    Lakini sijakata tamaaaa
    Isolate tamaaa bado nina vyeo kibao
    Ila usiache kunipigia debe ukikosa leo subiri kesho
    Nina majipu mengi ya kutumbua
    Wabeja nkoyi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad