Wastara Amnasa Kigogo Morogoro

IMEVUJA! Safari za mara kwa mara mkoani Morogoro, zinazofanywa na staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma zinadaiwa kuchangizwa baada ya kumnasa kigogo mmoja mkoani humo.

Chanzo makini kililiambia Risasi Mchanganyiko kuwa muigizaji huyo amempata mfanyabiashara na kiongozi wa serikali mkoani humo, kitu kinachomfanya afanye safari zaidi ya mara nne kwa mwezi.
“Yaani siku hizi Wastara hatulii Dar ilipo familia yake, amekuwa akisafiri Morogoro kila kukicha, yaani hivi sasa ni mapenzi motomoto, lakini ni kwa siri sana hataki ijulikane,” kilisema chanzo chetu hicho.
Baada ya kuunyaka ‘ubuyu’ huo, paparazi wetu alimtafuta Wastara na alipopatikana, alikana taarifa hizo na kudai safari zake za mara kwa  mara mkoani humo ni kwa vile huko ni nyumbani kwao.

“Hizo habari siyo kweli, watu wanapenda tu kuongea, Morogoro huwa naenda kwa sababu ya mambo mawili, kwanza kule ndiko nilikozaliwa hivyo huwa naenda kuwaona ndugu zangu na pili huwa naenda kwa sababu nina kituo cha kulelea watoto yatima, kwa hiyo huwa naenda kuwaangalia,” alisema Wastara.

Source:GPL
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pozi yako ni romantic sana Wastara

    ReplyDelete
  2. Jamani Lowassa si alikuwa juzi Morogoro???? Ama ikoje ikoje. Au ndio aliishamtanguliza Mamaaaa???????......Kwa maana hawa watu wa vyama vya upinzani nao kwa kweli ni shida. Lakini isiwe tabu acha Lowassa ajilie vyake lol!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad