Watanzania wengi wapo gerezani Afrika Kusini kwa ‘unga

WAZIRI wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga amesema Watanzania wengi wanashikiliwa katika magereza ya Afrika Kusini kwa makosa ya kujishughulisha na biashara ya dawa za kulevya.

Alisema hayo wakati akifafanua suala la Watanzania wanaoishi nje ya nchi, hasa vijana na kusema wamekuwa wakijishughulisha na uuzaji dawa za kulevya badala ya kuwa raia wema.

Aliwataka kuacha kujishughulisha na mambo yanayoweza kuwaweka kwenye wakati mbaya na kutii sheria za nchi waliko.

Alisema Watanzania wengi waliopo Afrika Kusini wanafanya kazi ya kusafirisha dawa za kulevya na wengine wanasubiri ‘kuzamia meli’ mjini Durban.

Alisema suala hilo ni moja ya mambo ambayo yamekuwa yakijadiliwa na Serikali ya Afrika Kusini ambapo Tanzania imejulishwa tatizo hilo na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Afrika Kusini pamoja na Rais Jacob Zuma.

“Ni kweli lipo tatizo kubwa la Watanzania waliopo Afrika ya Kusini kujishughulisha na biashara ya dawa za kulevya. Serikali ya Afrika Kusini imetujulisha jambo hilo nasi tunalishughulikia kuiepusha nchi kuwa na uhusiano mbaya wa kidiplomasia na nchi nyingine.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. JK alikuwa na majina ya vigogo wauza UNGA kakaa nayo miaka 10
    Kaondoka nayo na hata hajayakabidhi kwa awamu ya Tano hadharani Kama alivyofanya kwenye Mali za CCM
    Watanzania haituingiliii akilini
    Serikali inaposema kuna watanzania wamefungwa kwa ajili ya madawa ya kulevya nchi za nje
    Wakati hadi leo majina hayajatajwa
    Yetu macho mtaficha moto lakini moshi tutauona

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad