Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Waziri Nape amesema kuwa vituo hivyo kwa nyakati tofauti zilitangaza habari ambazo ndani yake zina uchochezi.
“Adhabu hii ya kuvifungia kwa muda vituo hivyo viwili inaanza leo (Agosti 29 2016) hadi pale kamati itakapomaliza kazi yake,” alisema Nape.
Aidha, amesema kuwa ameiagiza Kamati ya Maudhui ya vyombo vya habari kuviita vyombo hivyo na kuvihoji kwa kina kisha kumshauri hatua zaidi ya kuchukua.
Waziri huyo ameeleza kuwa Serikali inaendelea kutambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika kuleta amani na ushirikiano nchini na sio vinginevyo.
Hivi karibuni, Nape alitahadharisha kuwa vyombo vya habari vitakavyoripoti taarifa ambazo ni za uchochezi vitakumbwa na rungu la kuhusika kwa uchochezi pia.
Tutaona Mengi mpaka uongozi huu kumaliza MDA wake
ReplyDeleteHongera sana Mh. Nape. Jukumu tumekupa na utekelezaji unao. Na tahadhari umeitoa na kuiweka Bayana. Sasa hawa wanojifanya Hamnazo wajaribu na Tutawashughulikia.
Deletefala sana hy lapelape
ReplyDeleteMtafunga magazeti, vituo vya habari, watu, then what. Huu ni woga wa ccm. Badala ya kujadili matatizo mbatumia nguvu.shows your weaknesses and fear in leadership.
ReplyDeleteMtafunga magazeti, vituo vya habari, watu, then what. Huu ni woga wa ccm. Badala ya kujadili matatizo mnatumia nguvu.shows your weaknesses and fear in leadership.
ReplyDeleteJamani Magic FM wamekosa nini? Alosikia hayo maneno ya kichochezi hebu atuambie tafadhali!
ReplyDeleteHongera sana Mh. Nape. Jukumu tumekupa na utekelezaji unao. Na tahadhari umeitoa na kuiweka Bayana. Sasa hawa wanojifanya Hamnazo wajaribu na Tutawashughulikia.
ReplyDelete