Wema Sepetu Amenishangaza Kwa Kauli ya "Mimi na Uzungu Wangu"

Jana usiku katika taarifa ya habari ya TV1, habari ikielezea uhamasishaji wa wasanii kuupa kipaumbele miziki yenye mahadhi ya uswahili kama segere na singeli nimemsikia Wema Sepetu akihojiwa na kuzungumza haya:-

"Mimi pamoja na uzungu wangu lakini huwa napenda nyimbo zenye uswahili kama hizi"

Kwa aliyeelewa vizuri hiyo kauli ya Wema ilimaanisha nini? Je Kweli Wema ni Mzungu?

Nawasilisha.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Weeeee nae kichefu chefu kwani wema kusema uzungu ndo ina maana ni mzungu kwa rangi na kabila au...neno uzungu linetumika kuonesha aina flan ya maisha yake anayoishi japo ye ni mswahili pyuuua lakn mambo ya kisw hanaaaa katawaliwa na uzungu kuanzia roho yake mpka matendo...japo ye si mzungu...nikisema uswahili namaanisah unafki chuki zisiZoisha kutojua kusamehe haraka kuweka mavinyongo kuchambana hovyo...vita zisizOkuwa na maana...kwa wema vyote hivyo hukuti ndo uzungu wake sasa...

    ReplyDelete
  2. Hayo Ni maoni yake sijaona kibaya alichongea

    ReplyDelete
  3. Uzungu upi?
    Kusema uongo
    Kujisifia
    Anaiga ya wazungu si mzungu wala shombe wala zeru zeru
    Mswahili wa mazense
    Mshamba mkubwa

    ReplyDelete
  4. Kwani wazungu wana nini zaidi yetu, mzungu ndie always yuko right! Imefika mda sisi weusi tujue samani yetu

    ReplyDelete
  5. Niwasaidie amemaanisha nini;

    Uzungu

    1. Anapenda kuongea kizungu
    2. Hu kiss wanaume hadharani kama wazungu
    3. Anavaa wigi au kushonea nywele awe kama mzungu
    4. Alilelewa kwa muda fulani ktk mazingara ya uzunguni.
    5. Hana umbea umbea bifu bifu za Waswahili ila bifu wanaletea.

    Uswahili
    1. Anapenda madiko diko (chakula) ya Kiswahili
    2. Anapenda ngoma, nyimbo, kangamoko za Kiswahili
    3. Ana ndugu wengi waswahili dar, singia na znz
    4. Anarandana na ma D.
    5. Anapenda wanaume wadogo Waswahili ma mabuzi

    Hapo uzungu imezidi? Kweli na uzungu wake bado tabia za Uswahili anapenda. Kwa mchanganyiko huu she is a better person maana anafit kote na hana dharau. Si sawa na Zari.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad