Wema Sepetu: Niacheni jamani Nimechoka

Wema Sepetu 
Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ameonesha kuchoka na maneno mbalimbali kutoka kwa watu hususani kwenye mitandao ya kijamii kiasi cha kuamua kutoa yake ya moyoni kwa watu wote ambao wamekuwa wakimfuatilia maisha yake.

Ameonesha kukasirishwa na baadhi ya watuwanaomsema kwenye mitandao ya kijamii hususani kuhusu mapungufu yake.

Wema Sepetu ametumia mtandao wake wa Instagram kuweka ujumbe mrefu kwa watu hao, huku akiwataka wamuache aishi maisha yake kwani hajawahi hata siku moja kwenda kuomba msaada kwao, na kusema hata siku atakapokufa atakufa mwenyewe na kama ni majibu kwa Mungu atajibu mwenyewe.

“Naomba niseme kitu na nieleweke tafadhari, sijawahi hata siku moja kwenda kwa hata mmoja wenu na kumgongea kuomba hata hela ya chumvi. Maisha yangu yananihusu mimi na hata siku nikifa nakufa mwenyewe, majibu kwa Mungu naenda kujibu peke yangu. Niacheni jamani nimechoka” aliandika Wema Sepetu

Mbali na hilo Wema Sepetu amewataka watu ambao wanakereka na aina ya maisha ambayo yeye anaishi waache kuyafuatilia kwani si lazima kufuatilia kile akifanyacho au maisha anayoishi yeye.

“Kama nakukera na maisha yangu basi usiyafuatilie siyo lazima. Nisiheme sasa jamanii. Naomba tafadhari kama mapungufu ni ya kwangu mimi. Niacheni mimi nafanya kile kinachoridhisha nafsi yangu maana sipendi kujikasirisha. Kwani nikitajirika mimi au nikiwa masikini wewe unapata faida gani. Jiulize kwanza hilo swali ndiyo uanze kutoa maneno yako” alisema Wema Sepetu

eatv.tv

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. funga a/c zako kwa muda dada!

    ReplyDelete
  2. Na wewe Wema kwa nini hudharau hayo na ukakaa kimya? Tumechoka na hizo comments zako za kila siku. Nimekuona jana airport unaelelekea SA. Nafikiri bila hayo ma wig unayovaa na make up unavyojipaka wewe so mzuri kama unavyopenda watu wakufikirie

    ReplyDelete
  3. Wema ni mzuri periodddd...make up ni urembo tu kajiongezea nadhan hujawahi kumuona bila make up...she is soo beautiful... baada ya kuacha kutumia mkorogo

    ReplyDelete
  4. wewe Anonymous hapo juu kwani hujawahi kumuona wema kwenye tv kwenye kipindi chake bila mawig na bila makeup mbona ameonakana mara nyingi tu mpaka ameonekana kipara katika tv sio kwamba Wema anajificha na mawigi na make up ili watu wamuone mzuri sababu tumeshamuona bila mawigi na make up na wema yuko mkweli mbona wasanii wengi hata akina Beyonce bila mawig na make up hawaonekani kivile kama watu wanavyofikiria au wanavyomjua siku moja Beyonce alitoa wigi lake dunia nzima watu walishangaa hakuonekana kabisa kama beyonce ambavyo watu walivyozoea kumuona mpaka watu walimwambia arudishe tena wigi lake kichwani

    ReplyDelete
  5. na wewe tuonyeshe uso wako uliokakamaa kama kona ya kitanda. Wema anakunyima usingizi tuu. sema ukweli.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad