ACT – Wazalendo Yatabiri Uchumi Kuporomoka

CHAMA cha ACT – Wazalendo kimesema katika kipindi cha miezi sita tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, uchumi wa taifa umeporomoka kwa asilimia nne.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, akinukuu taarifa ya Benki Kuu (BOT), alisema katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba mwaka jana, pato la taifa lilikua kwa asilimia tisa. Lakini kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu, limepungua na kufikia asilimia 5.5.

Alisema kulingana na mwenendo wa uchumi, Kamati Kuu ya chama hicho imeitaka Serikali izingatie sayansi ya uchumi katika kuendesha nchi.

Zitto alisema uamuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kuitelekeza Serikali kwa mwanasiasa mmoja na kudhani ndiye anayejua kila kitu na kuwa mshauri wa washauri wa uchumi, itasambaratisha uwekezaji nchini na kuua kabisa juhudi za miaka 20 za kuvutia uwekezaji na kujenga uchumi shirikishi.

“Tunawahimiza wananchi kuzingatia kuwa msingi wa uchumi wetu ni uwekezaji kutoka ndani na nje ya nchi, hivyo msingi wa kuvutia uwekezaji ni utawala bora. Serikali ya CCM inapaswa kujua kuwa kuua utawala wa sheria ni kuua uwekezaji pamoja na uchumi wa nchini.

“Tangu kuingia kwa awamu ya tano, Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi imekumbana na changamoto ya uchumi kukua bila kuwanufaisha wananchi wa kawaida, wakati tulitegemea Serikali mpya ingeanza na kukuza uchumi wa taifa.

“Hali hiyo inamaanisha kuwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo wa  awamu ya tano umepungua kwa asilimia 4,” alisema Zitto.

Zitto ambaye alikuwa akitoa msimamo wa Kamati Kuu ya chama chake iliyoketi juzi Dar es Salaam, alisema katika sekta ya kilimo ambayo hutegemewa na wananchi kwa asilimia 70, pato la uchumi limezidi kushuka kutoka kasi ya ukuaji wa asilimia 10 kwa robo ya mwisho wa mwaka jana hadi kufikia asilimia 2.7 katika kipindi cha Januari hadi Machi, mwaka huu.

“Watu wameishiwa na imani kuendelea na shughuli za ujenzi, mfano nyumba zilizokuwa zikijengwa zimeachwa kujengwa,” alisema.

Habari hii imeandaliwa na Herieth Faustine, Johanes Respichius na Pauline Kebaki (Turdaco).

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ACT achane siasa za majitaka mara uchumi mara kubaniwa demokrasia hivo mnayoyasema ya kila mtu ashauri wake na ufanyiwe kazi na raisi je raisi akae na kupoteza wakati kusikiliza ushauri itamchukua miaka mingapi anze kutimiza kwa sababu sio nyinyi tuu mnaotaka kusikilizwa kuna watanzania wengi tuu wanataka kutoa michango yao kuishauri serikali hizo ndio sababu zitafanya uchumi wa nchi kushuka uchumi kushuka mwacheni Magu afanye kazi hakuna serikali ndani ya serikali subirini mchike dola sijui mtatupeleka wapi

    ReplyDelete
  2. Jito.. Si Nilisikia umeoa!!! haya wewe na takwimu za uchumi wapi na wapi? au ndiyo ulivyo fundwa. Nani alikwambia sisi ndiyo tunawashauri wachumi kama wewe.. Unajiweza. Unamkusudia nani mjua kila kitu... Jito ..Jito Upo mwanangu.. Barida. Tudondoshee kitu wanachana na haya... Viwanja vinawenyewe watajenga Tu. Kumbuka Nguvu Jasho HAPA NI KAZI TU

    ReplyDelete
  3. Jamani.... Shehe Yahaya Hussein si tulimzika.. Sasa huyu mtabiri anaezuka sasa katokea wapi? au ndiyo viroja vya ulimwengu?

    ReplyDelete
  4. Kiongozi Mkuu... Wa Wapi?

    ReplyDelete
  5. Go to hell wewe kimbelembele wa kila kitu kudadeki sasa"dili"zenu zilizokuwa zinawapa jeuri zimezibwa kwa aina moja au nyingine maionja joto ya jiwe kidogokidogo mnaanza kuropoka ropoka hovyo Magu kaza tena buti kisawasawa kudadeki zao waisome namba

    ReplyDelete
  6. Watu walikuwa wanajenga nyumba kwa sababu ya hela za wizi kutoka Serikali. Sasa huo wizi hakuna tena na Serikali imeamua kubana matumizi. Sasa hicho kitu kinawauuuumaaaa mpaka mapovu yanawatoka na mnaishia kutoa takwimu zisizo kuwa na kichwa wala miguu. Huo mchanganuo wako wewe Zitto Kabwe na Chama chako ni wa kisiasa zaidi na sana sana kumshambulia Rais JPM kama ilivyokuwa kawaida yenu. Hamna lolote lile na wala hamkuzingatia mchanganuo wa kiuchumi. Imekula kwenu mwaka huuuu na mtaisoma namba sana tu.

    ReplyDelete
  7. hivi NYINYI VIONGOZI WA VYAMA PINZANI AKILI ZENU ZIMEKALIA WAPI???Angalia hii!“Watu wameishiwa na imani kuendelea na shughuli za ujenzi, mfano nyumba zilizokuwa zikijengwa zimeachwa kujengwa,” alisema.JIBU ALISHATOA MH.Rais.MAGUFULI..HAO NDIO WALIOKUWA WANACHOTA FWEZA ZA WALALAHOI.NAKUJILIMBIKIZIA,nini hao wengi wao wameyakalia manoti chini ya magodoro..ndo maana akataka abadilishe NOTI..

    ReplyDelete
  8. Uchumi ukiporomoka wa kulaumiwa nani kama siyo kila mtanzania.haya madudu baki nayo mwenyewe Zitto maana tumewachoka mno wapinzani hamna jema

    ReplyDelete
  9. Hatakama unaumia kama unaamini utafanikiwa kwa yule umuaminiye huwezi waza tofauti, Hivyo imani juu ya kitu au mtu UDUMAZA uwezo wa kufikili na kuchanganua kitu au mtu husika.

    ReplyDelete
  10. Zitoo, Mimi sins hata la kuchangia. Mannake nakuelewa wewe mtafuta kiki za mitandao. Unanichefua natamani kutapika. Unanitika kichefu chefu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad