ATCL Kuanza na Kosa la Kwanza
9
September 30, 2016
ATCL kama yalivyo mashirika mengine ya umma, kila mara imekuwa ikizaliwa na kufa kutokana na muundo wake usiokuwa wa kibiashara. TANESCO isiyo na mshindani yeyote, TTCL ambayo awali haikuwa na mshindani, na mengine mengi yaliyokwishakufa na yaliyouzwa, mashirika yote hayo yalikufa kwa sababu yalianzishwa, kuendeshwa na kusimamiwa kiserikali/kisiasa.
Serikali haijawahi kuendesha biashara ikafanikiwa. Tatizo linaanzia kwenye muundo wa haya mashirika/makampuni. Wanasiasa/viongozi wa serikali ambao kimsingi si wafanyabiashara ndiyo waliotengeneza muundo wa uendeshaji na ndiyo wenye kauli ya mwisho. Vigezo vya wajumbe wa bodi na watendaji wakuu wanavyo wao. Na siku hizi PhD imekuwa ni kigezo kikubwa sana ingawa kiuhalisia, kwa Dunia nzima, ni nadra sana kuwaona wenye PhD wakiwa wafanyabiashara wazuri na waliofanikiwa.
Juzi wakati Mh. Rais akizindua ujio wa ndege mpya alisema ATCL imezaliwa upya, ina ndege mpya, bodi mpya na uongozi mpya, sikusikia kama ina muundo mpya wa uendeshaji na usimamizi. Bado inaonekana ATCL itandeshwa kwa mkono wa serikali.
RAIS - 'ATCL ISITUMIE MAWAKALA WA KUKATISHA TIKETI'
Hili tayari ni agizo ambalo naamini ni agizo lisilo sahihi. Tayari serikali imeanza toka hatua za mwanzo kuingilia uendeshaji wa ATCL. Rais anapoagiza ATCL isitumie mawakala wa kukatisha tiketi inamaanisha ATCL iwe na wafanyakazi waajiriwa kila mahali nchini. Gharama za maelekezo hayo itakuwa kama ifuatavyo:
ATCL italazimika kuwalipa wakatisha tiketi mishahara, matibabu, posho, michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, usafiri, n.k. ATCL italazimika kulipia gharama hizo zote bila ya kujali mkatisha tiketi anakatisha tiketi ngapi au kama amepata wateja au hakupata kabisa
ATCL italazimika kulipia ofisi na kuweka miundombinu ya ukatishaji ticket nchi nzima. Ifahamike kuwa ukitaka kuwa na ufanisi unalazimika kuwa na ofisi za ukatishaji tiketi hata mahali ambapo ndege haitui, kwaajili ya kuhudumia abiria wanaotoka maeneo hayo wanaotarajia kutumia usafiri wa ATCL kutokea uwanja ulio karibu
ATCL italazimika kuwapa mafunzo wakatisha ticket watakaotapakaa nchi nzima
Wakati ATCL watakapokuwa wanahangaika na kuwa na wakatisha ticket wao na ofisi zao, washindani wao wataendelea kuwa na wafanyakazi wachache, wakiwa na mawakala wengi wanaolipwa kutokana na idadi ya ticket na thamani ya ticket walizokatisha. Hawalipii ofisi, hawalipii matibabu, hawalipii michango ya hifadhi ya jamii, hawalipii likizo ya mfanyakazi. Mawakala wao wanalipwa kutokana na wanachozalisha, wasipozalisha hawalipwi chochote.
ATCL wanaanza na quandary ya kwanza, wafuate maagizo ya mwenye mali au kanuni za biashara? Je, hii ni ya mwanzo na ya mwisho au zitaendelea kuja na nyingine? Kwa kuwa tatizo la msingi la uendeshaji biashara zilizo chini ya serikali halijatatuliwa, haitakuwa jambo la ajabu ATCL kufuata projectile ya mashirika/makampuni ya umma.
By Msambichaka Mkinga
Tags
well said......words of the wize.........biashara ina wenyewe
ReplyDeletedu hii inawezekanaje?
ReplyDeleteKwanza ningekushauri kaka ungefanya Equilibri kabla ya kuraumu serikali,i mean ungeweka research ulio ifanya wakati Shirika la ATCL likiwa na wafanyakazi 500 wakiwa hawana ndege hata moja wakitumiandege zenye uwendeshaji wa gharama kubwa tena pasipo na kauli ya kiongozi yeyote wa kiserikali i mean walikua free kama hivyo ulivyo sema kua sasa inaonekana serikali inaingilia masuala ya kitendaji ya shilika pasipo na utaalamu wa uwendeshaji yaani ukimaanisha kua serikali haina utashi juu ya masuala ya uwendeshaji wa Mashirika yake na iwaachie brokers waliendeshe Shirika la Serikali kwa uwelewa wako kaka,hii si kweli kwanza unapaswa kujua kua Serikalini Mfano wa Baba aliempa pesa mwanae akafanye biashara na sidhani kama wewe ni baba utakubari uumpe mtoto wako mtaji kwaajili ya kufanya biashara pasipo na wewe kama mzazi kumpa muongozo mtoto wako,kwamaana hiyo wewe kama mzazi hauna akili.Lets back to the point kwanza kama utakua umenielewa mfano wangu utakue uneshaelewa kua ni nini kua naongelea,Serikali ndio imeamua kutoa pesa zake na kuziazimisha katika Shirika la ATCL ili Shilika liweze kujiendesha na kuirejesha pesa ya Serikali.sasa sijajua ulikua unamaanisha nini juu ya hii makala yako kaka
ReplyDeleteMhh Muandishi umenena haswa...
ReplyDeleteNi kweli changamoto ni kubwa kuliko tunavyoona,lazima tuwe na wataalamu ambao wana uzoefu na biashara hii,kwani kuna makampuni makubwa ya ndege ambayo yanauwezo kifedha, wamejikuta wanashindwa kufanya biashara hii. we must be strategic kuweza kuendelea kuwepo kwenye biashara hii. kupata ndege ni moja kati ya mambo mengi yanayotakiwa kufanywa. Mwenyezi Mungu tupe uwezo wa kila jambo ili ndoto hiyo itimie.
ReplyDeleteRaisi inabidi awe na mshauri aliyezamia mambo ya uchumi mwenye experience. Huwezi kufanya kila kitu.waachie wenye uzoefu kwa mambo kama haya.
ReplyDeleteRaisi inabidi awe na mshauri aliyezamia mambo ya uchumi mwenye experience. Huwezi kufanya kila kitu.waachie wenye uzoefu kwa mambo kama haya.
ReplyDeleteNinachojua mimi ni kuwa JPM hawezi zungumza pasipo kujua anachozungumza.
ReplyDeleteBiashara ya ndege ni lazima ucheze na 3rd party mfano mzuri ni Fast jet pamoja na mafanikio wamebidi wafanye re structuring kwa ujumla mtaona wanatoka kwenye mfumo wa wet lease kwenda dry lease agreemennt i.e 3rd party busenis kwa kweli Mkuu alikosea kidogo hapo kwa mawakala,
ReplyDeletewakala ni mtu wa muhimu sana katika biashara hii anapunguza mambo mengi sana hata kiutawala bado chance ipo bado ATCL still wanaweza kufanya mashauriano na mambo mengine yanayohitaji taaluma ni bora kuwaachia wataaluma washauri!!!