Aunty Ezekiel Afunguka Sababu ya Yeye Kujiachia Enzi Zile

Nyota wa filamu nchini Aunty Ezekiel amefunguka kuwa kipindi cha nyuma kabla ya kuwa na mahusiano na Mose Iyobo na kabla ya kupata mtoto alikuwa akijiachia sana kwa lengo la kutafuta kiki na wala hakuwa na woga wa kufa kwani hakuwa anategemewa na mtu.

Aunty Ezekiel alisema hayo kwenye kipindi cha eNewz na kudai kuwa alikuwa akivaa vibaya na kuwa na skendo mbalimbali kwa lengo la kutafuta kiki na kufahamika zaidi lakini saizi yeye hafanyi tena mambo hayo kwani amekuwa akiogopa kifo kwa kuwa anatambua nyuma ana mtoto ambaye anamtegemea na anategemea malezi yake, ndiyo maana ameamua kuachana na mambo hayo.

“Kwa sasa nimeacha kiki za ajabu ajabu saizi naangalia maisha ya familia, saizi nimekuwa mama naangalia vitu kwa upande mwingine kesho na kesho kutwa mwanangu amekua, amekuta hayo matukio, ohh mama yako alivaa kichupi, mama yako alikuwa hivi alikuwa vile ataiga nini mtoto kutoka kwangu? Kwa hiyo saizi naangalia mara mbili ya pale nilipokuwa mwanzo. Hata zamani nilikuwa ni mtu ambaye nasema aah si tunaishi mara moja tu hivyo kesho na kesho kutwa nikifa nasema potelea mbali lakini saizi nakiogopa kifo kutokana na kwamba nina mtu nyuma yangu ananitegemea” alisema Aunty Ezekiel

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na binti yako pia atafuata nyayo zako atakapokua ataanza kwa kutafuta kiki kwanza then akizaa ndipo atulie, like mother like daughter

    ReplyDelete
  2. Sio anamuagopa Mungu? watu wangine utadhani wamejiumba wenyewe!! Mimi nilifikiri atasema sasa nimeamua kumrudia Mungu hivyo nimeacha mambo machafu. Kwa hiyo alikuwa radhi kufanya uchafu wooote ule kwa sababau alikuwa hana mtoto! Mungu na mtoto nani zaidi, Jamani jamani watu wajichunguze mara mbili wakati wanaongea.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad