CHADEMA Wagoma Kuhamia Dodoma, Wadai Hawana Mpango Huo

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema wazo la kuhamia Dodoma halimo kwenye ajenda zake.

Akizungumza na Mwananchi hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji alisema chama hicho hakina mpango wa kuhamia Dodoma kwa sababu hayo ni masuala ya kisiasa yasiyo na msingi kiuhalisia.

“Sisi makao yetu makuu yapo Dar es Salaam, hata katiba yetu ndivyo inavyosema, tutaendelea kuwa hapahapa. Hayo ni mambo ya kisiasa yasiyo na misingi ya kiuhalisia, hata mazingira hayaruhusu, kwa hiyo sisi tutaendelea kuwa hapa (Dar es Salaam),” alisema Dk Mashinji.

Chama cha ACT Wazalendo kilisema kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi ni miongoni mwa ajenda zake.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Makao Makuu ya CHADEMA kuhamia ARUSHA ni bomba sana kwani viongozi wote wa ngazi ya juu kwa 99% tunatokea Arusha hivyo kuhamishia makao ya chama chetu Arusha itatusaidia sisi kufanyia kazi nyumbani au karibu sana na nyumbani
    Jamani Halima Mdee yuko wapi tuna m-miss sana mwanaharakati wetu.

    ReplyDelete
  2. Uhamie usihamie mimi nimesharudisha Kadi ile ya chadema.. Baada ya kuona Vioja vya miliowapa kura na kukimbia vikao wanaingia misheni tauni kufanya madili yao huku hawaniwakilishi.. Isiwe tabu mkae hai au matombo na ikibidi hata msolwa nyie kaeni tuu. Hamzidishi wala...............nguzi. Magu Kazi buti na spidi ile ile. Mungu akulinde JPJM

    ReplyDelete
  3. Chadema haiwahusu kuhamia Dodoma ni hiari yao kuhamia sasa hilo la kugoma linatoka wapi ingekuwa wameambiwa kuhama hapo sawa suala la kugoma lingewahusu

    ReplyDelete
  4. Mbona Chadema wanarukia rukia kila kitu lazima waseme inawahusu nini ya kuhamia Dodoma na wamekuwa serikali

    ReplyDelete
  5. Kitu cha kushangaza Chadema nikung'ang'ania vitu visivyo kuwa na msingi wanachofikiria sasa kuwa magazeti yanawabeba na kuwapa umaarufu kwa kuwapambia habari zao kumbe ndo wanawamaliza kabisa kisiasa Duh jamani watu walishaichoka Chadema na mavituko yao inaonekana kama chama cha kitoto ingawa kuna watu wazee na akili zao wameshindwa kugeuza upepo yaani chama kinameguka wakikumbuka shuka kumeshakucha

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad