Chereko za Wimbo wa Salome zisimlize Tena Saida Karoli

Anga la burudani nchini hivi sasa lipo kwenye msisimko wa tenzi ya Wasanii Diamond Platnumz na Raymond ambao wameachia songi la Salome, ambalo ni marejeo ya songi pendwa lililloimbwa na dada yetu wa Kihaya, Saida Karoli, liitwalo 'Maria Salome' almaarufu 'Chambua kama karanga'..

Tumeona uongozi wa WCB chini ya Diamond ukijitoa lawama kwa kuonyesha kuwa kuna makubaliano ya kuurudia huo wimbo baina yao na Dada Saida kupitia menejiment yake.

Sasa hii ni mara ya 3 huu wimbo unatumika kimaslahi. Mara mbili zote zilizopita zilionyesha kama dada hakuambilia kitu licha ya watu wa pembeni kudaiwa kupiga hela ndefu..

Diamond, mshike mkono Saida. Wajanja wasije wakatumia tena ujanja wa makaratasi wakamlaza njaa.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Well done Platinum, hakuna njia nyingine ya kuwaenzi wasanii waliopita kama ulivyofanya kwa wimbo huu wa Saida Kalori, lakini pia ni faraja kwa wakazi wa Mkoa wa Kagera kwa mkasa uliowapata hivi karibuni kwani ujio wa wimbo huo umekuwa kama mlipanga lakini najuwa ni mapenzi ya mola. Kama kutakuwa na vijisenti basi mkumbukeeni mwana mama huyo naamini sasa anaangaika na maisha kivingine.Wasanii na wanamziki igeni kama alivyofanya PLATINUM mwisho wa siku tutafika salama.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad