Diva:Mastaa wa Bongo Waelewe Thamani yao, Mimi Nachaji Milioni 3.5 Kwa Appearance tu

Mtangazaji wa Clouds FM, Diva The Bawse amewataka mastaa wa Tanzania kutambua thamani ya brand zao na kuacha kujichukulia poa.


Amedai kuwa mastaa wengi wamekuwa wakitumika bure kufaidisha watu wengine na anadhani ni muhimu wakaacha kujishusha kiasi hicho.

Anadai kwa upande wake yeye, hafanyi kitu bure na kudai kuwa hata kuonekana kwenye saa moja kwenye party ya mtu, ni lazima awe amemlipa.

“My standard rate is 3.5 million in one night that including 30 minutes hosting, na sikai less than hour naondoka,” Diva ameandika kwenye blog yake.

“Ifike stage celebs wajue value yao na sio kutumika tu kwa faida ya watu wengine. Chochote unaona pia napost kwenye account zangu za mitandao kinalipiwa., lazima ujue kama wewe ni maarufu lazima ulipwe hata kutweet brand ya mtu mwingine,” ameongeza.

Mtangazaji huyo ana zaidi ya followers milioni 1.1 kwenye Instagram na amekuwa akiingiza mkwanja mrefu kwa kupost matangazo mbalimbali.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿😂😂😂😂😂😂😴😴😴😴😴😴😴🍻🍻🍻🍻🍻🍻😹😹😹😹😹😇😇😇😇😇😇😇😇😇😇😇😜😜😜😜😜😜😎😎😎😎😱😱😱😱😱😭😭😭😭😭😭😷😷😷😷😷😷😷😷

    ReplyDelete
  2. Ndio kusema kwenye vigodoro na vigoma weye huendagi?? Basi pouwa

    ReplyDelete
  3. nani atakulipa milion 3 na nusu hata bongo Movie kwenyewe wengi wao wasanii maarufu hawalipwi namna hiyo ndiyo itakuwa wewe kwanza wengi hawakujui wewe ni nani, na unajiita msanii kwa lipi? mbona wewe ni kawaida tu,hata Wema mwenyewe aliye maarufu kuliko wewe halipwi hela kubwa namna hiyo kwa just show up. kama angekuwa analipwa kiasi kama hicho basi angekuwa tajiri sana leo na wala asingeiba umeme

    ReplyDelete
  4. Tuko USA nadhani sio Africa, USA kwenye mambo ya dolla, watu wanajiona babkubwa, hata hiyo chage ya huko, ni kulingana na maisha yao, huku bongo ikichenjiwa watu heeeee!!!! Wanasahau ya kwetu ni madafu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad