Inawezekana Hatumuelewi Rais Dkt. Magufuli..ila yeye Anazidi Kuchanja Mbuga

Amani iwe kwenu!

Nimejaribu kutafakari kidogo juu ya kauli kadhaa za rais wetu akiwa katika baadhi ya ziara na kubaini kitu..
1. Inawezekana kauli tata za mh. ni za makusudi na zinalengo la kubadili sura nzima ya siasa tulizozoea..Hii nikiwa na maana kwamba wakati tukiwa bize kujadili kauli tata hizo teyari yeye anapata mwanya wa kufanya mambo ya msingi ambayo anatarajia kuyafanya!Ni kama unaweka nyama na wakati huo huo unampigia mluzi mbwa..lazima aweweseke!

2.Kauli zake nyingi pia zina vichekesho na mikwara mingi..Hii mikwara inaweza kuwa na lengo la kuwaweka sawa watendaji au watu waovu!Kwa jinsi navyoona haya yote anayafanya makusudi kwa kuamini kwamba meseji zinafika na watu wanamsikiliza neno kwa neno!

3.Kwa kuzingatia kuwa watanzania na wanasiasa ni watu wa porojo na propaganda basi naona anacheza kama pele kwenye hili na wanasiasa wengi hawajamstukia!Vyama vya upinzania visipokuwa makini vitabaki kujadili hotuba zake badala ya kujikita kwenye main agenda za vyama vyao..

4.Pia muheshimiwa kuna wakati kwenye hotuba mambo ya sirini huyaweka wazi wazi..Nahisi anafanya makusudi kuwa hata wale wanaofanya maovu na kusitiriwa kisiasa basi kuna siku watawekwa hadharani..amefanya watu wa deal na wala rushwa kubwa kuwa waangalifu maana kuna siku wanaweza kusemwa hadharani..Miaka ya nyuma hatukuzoea hii na tunaona kama wanadhalilishwa..

5.Tukumbuke rais wetu ni msomi wa Phd na si bure lazima huwa anajitafakari baada ya hotuba zake lakini pamoja na hilo bado wimbi la kauli tata linaendelea na bila shaka ni makusudi kwa lengo maalum kwa kuzingatia aina za siasa tulizozoea..Yaani huwa anapiga pale pale tunapoona amekosea au atakosea na mbaya zaidi huwa haachi kurudia pale anapoona watu wamekwazika!

Kitu ninachokiona ni kuwa rais anataka kututoa kwenye aina za siasa tulizozoea,yaani analeta a new era of politics!Wito wangu kwa viongozi wa upinzani na wanaharakati kama kweli mnataka kuisaidia hii nchi mjikite kwenye ajenda zenu na si hotuba zake kwa vipande hasa vyenye utata!Atawapoteza na wakati huo huo yeye anaendelea kuchanja mbuga kisiasa na kwenye ajenda zake..In short I can call him as a game changer and a smart president..

By Sonaderm/JF
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na achange mbuga Hana mpango wala shukurani ana nini
    Msukuma wakutuletea sisi
    Hao Pemba ya Pemba unguja ya waungunja
    Waliletwa toka tabora fyuuuuuuuu

    ReplyDelete
    Replies
    1. hapo unakosea Mdau. Ukitaka pemba ya asali na Unguja ya Maziwa.. Msikilize na mtii na umfuate JPJM .. Matokeo yake utaona mpaka Gesi itatolewa Pemba! au Hujui kama kuna Petrol na LPNG.. Usiwe na Chuki ili tujipange na kuleta maendeleo. Wewe ni wa wapi? Kaole au !!

      Delete
    2. Mdau, Nakusifu lisai kikubwa ni kwamba Mh. Raisi is genuine Person.. with no known prtocals or Unaweza kumtabiri. Na anonesha kuto kuwa na mihimili ya Rafiki. He potrays a straight and effective leadership unmatched. Mchezo hataki na wala hauvumilii uwe ni rafiki au kando ya pili. He Aims into an achivment leadership outspoken and full of pre warning if you do not Perform when he gives you a role.
      Umejitahidi katika kumueleza pia ndani ya hotuba zake ana break the ice kwa vichekesho.. i reality is a strong Message to the stake holders that we mean business that is not a business as usual. This is new Era Which he transform and change it completely. Magu has proved to be the ROLE MODEL IN AFRICAN LEADERSHIP. MAGU IS UNIQUE AND UNDERSTAND HIM NEEDS FOCUS AND PATIENCE.. ONLY THEN YOU CAM MARCH WITH HIM. OTHERWISE UTADUWAA NA KUSHANGAA UKITAHAMAKI MAGU AMESHASONGA MBELE NA TAIFA LINAENDELEA NA UTABAKI KUJILAUMU KWA NINI SIKUMUELEWA NA KUMPA USHIRIKIANO WANGU.. BORA TUAMKE SASA NA TUSHIRIKIANE NAE.. hAPA KAZI TU

      Delete
    3. Hahahahaha,na ndio rais wetu,ukubali ukae shauri yako.
      Rais ni mmoja tu,JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI.

  3. Uandishi wa kipuuzi kabisaa...penye ukweli watu watakosoa tu katiba ya nchi ifuate ma inafuatwaje sio kwa vitisho bali kwa utaratibu uliopo...muandishi huna ulichoandika hapo ziidi ya upupu...

    ReplyDelete
  4. TUNAMUELEWA SANA HATA KAMA NI KIMYAKIMYA.
    KUFICHA PESA KWENYE MAGODORO MAANA YAKE TUNAMUELEWA,
    KUWAHI KAZINI MAANA YAKE TUNAMUELEWA,KUTOKAA KWENYE BAA MUDA WA KAZI NDIO KUMUELEWA KWENYEWE,NA MENGI MENGINEYO.
    "HAPA KAZI TU"

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad