Kauli 10 Nzito Alizotoa Mbowe, Akiahirisha Ukuta

Mbowe
LEO mchana, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) taifa, ametangaza uamuzi wa kuahirishwa kwa maandamano na mikutano ya chama hicho nchi nzima iliyopangwa kuanza kesho, anaandika Charles William.

Zifuatazo ni kauli kumi zilizotolewa na mwenyekiti huyo wa Chadema, wakati akitangaza kuahirishwa kwa operesheni hiyo maarufu kama Ukuta, iliyotawala vyombo vya habari vya ndani na nje pamoja na mitandao ya kijamii kwa zaidi ya mwezi mmoja.

1.“Tunajua uamuzi huu utawaumiza sana wafuasi wetu, na uamuzi huu umeniumiza sana hata mimi mwenyewe, lakini ni nani miongoni mwa viongozi wetu na wanachama wetu ambaye anaweza kuombwa kuahirisha jambo na viongozi wa madhebu na dini zote hapa nchini na akawakatalia?”

2.“Polisi na Serikali wajue kuwa, hatuahirishi maandamano na mikutano yetu kwa sababu ya mazoezi, risasi au mabomu ya polisi. Hatuahirishi kwasababu ya usafi wao, wanaofanya kesho na wala hatuahirishi kwasababu ya ndege za kijeshi zinazoruka, ila tumeamua kuwaheshimu viongozi wetu dini.”

3.“Tunawaomba wanachama wetu, wapenzi wetu na wapenda demokrasia kote nchini watusamehe na wakubali kuwapa viongozi wa dini hizi wiki tatu, watafute suluhu kwa kuonana na Rais na ikishindikana, hatutarudi nyuma. Tutaingia barabarani.”

4.“Tangu tulipotangaza operesheni Ukuta, jumla ya wanachama na viongozi wetu 230 katika maeneo mbalimbali wamekamatwa na kushitakiwa kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo uchochezi na jumla ya viongozi na wanachama wetu 28 wapo rumande mpaka sasa pasipo sababu za msingi.”

5.“Haikuwa rahisi sisi kufikia uamuzi huu, hatukuwa tayari kurudi nyuma. Lakini viongozi wa dini na taasisi zinazoheshimika hapa nchini wametusihi. Mpaka Mama Maria Nyerere ameongea na Mheshimiwa Lowassa na kutuomba tuahirishe ili watafute suluhu ya suala hili.”

6.“Hatuogopi mabomu wala risasi za polisi, tuna uwezo wa kuandamana kwasababu tunazo mbinu za kufanikisha mipango yetu. Juzi polisi walitukamata na kuzuia kikao cha Kamati Kuu ila jana tumekifanya na wala hawajui tumefanyia wapi na saa ngapi.”

7.“Wakati tukifanya harakati hizi, tunaendelea pia kufungua kesi sehemu mbalimbali. Tundu Lissu na jopo lake tayari wameandaa mashitaka 15 ili tuweze kuyafungua katika mahakama zetu hapa nchini. Tutadai haki mahakamani na tutaidai barabarani.”

8.“Inasikitisha sana kuona taifa lina rais anayeomba watu wamuombee kila siku, ‘Niombeeni jamani’, lakini amekuwa akijaribu kuwakwepa viongozi wa dini kila wanapotaka kumuona ili kuzungumza naye kuhusu amri haramu ya kuzuia mikutano ya hadhara.”

9.“Viongozi wa dini walituomba wiki mbili au tatu ili wafanye mazungumzo na Rais Magufuli, sisi tumewapa mwezi mzima kabisa, ili wasake suluhu ili sisi kama vyama vya siasa tupewe haki yetu ya kisheria na kikatiba. Ikishindikana hakika sisi hatutarudi nyuma.

10.“Salum Mwalimu bado yupo rumande kwasababu za hovyo, Polisi wamekataa kumpeleka mahakamani leo wanadai wapo ‘busy’ eti wanazuia maandamano ya UVCCM, yalipangwa kufanyika leo. Sisi wote ni wafungwa watarajiwa lakini hatutarudi nyuma.

Post a Comment

16 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hapana Mbowe,usijidanganye na hiyo no.6 sio kwamba polisi hawakujua nini kinaendelea,na ujue humohumo kwenye kundi lenu wamo wapenda amani ambao wanapinga UKUTA hata labda kama wewe hujui.UKUTA haitakuwepo tunaendelea kuomba amani na utulivu.KAMPEI YA UKUTA ISHINDWE.

    ReplyDelete
  2. Lakini wananchi tunaangalia pia,Hivi Mbowe kwa utajiri ulionao ni msaada gani umetoa kusaidia serikali hata kidogo ukiwa kama mbunge?
    Tumeona akina Bulaya,sakaya,Haule wanatoa misaada kutuhamasisha tuliowachagua kwa nini wewe hufanyi hivyo?Watu wa vyama tofauti wanachangia madawati,mbona wewe huumii kuona mtoto anasomea chini?Sidhani kama una nia nzuri na UKUTA,naamini ni kuwavuruga wananchi wauponde uongozi uliopo madarakani,ili ujitengenezee njia ya kuwa mshindi 2020 na ni dhahiri kuwa una uchu wa madaraka,Haingii akilini jinsi ulivyo tajiri ukose ushawishi wa mchango kwa wananchi hata kwa asilimia kidogo,bora hata mh.Lowasa tumeona mchango wake.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sema mdau,CHADEMA hata usafi hawataki kushiriki,yaani jambo lolote linaloamriwa na serikali hawataki kushiriki,siwaelewi.

      Delete
  3. WEE BWANA UKO VIZURI NA HATA UKIFA LEO FAMILIA YAKO IKO NA ITABAKI NA NEEMA,MIMI NDIO NAANZA KUTAFUTA.KWELI UKUTA NI KUPINGANA NA DOLA.TUFIKIRIE,TUSIFUATE MKUMBO.

    ReplyDelete
  4. Mh.MBOWE mimi ni UKAWA lakini napingana na wewe mkuu,
    Ya kwamba tusishindane na serikali na tumpe muda Rais.
    wengi wanapinga hatua munazochukua chadema.

    ReplyDelete
  5. ni uonevu mtupu Tanzania hao polisi usiseme bora wangevaa tu mafulana ya mapicha ya bwana wao

    ReplyDelete
  6. Mbowe kiburi kitakumaliza kisiasa.

    ReplyDelete
  7. Endeleeni tu na mbwembwe zenu,kikubwa amani iendelee nchini kwetu.

    ReplyDelete
  8. Wengi walikuwa wanakereka na ukuta,nashauri hata hiyo oktoba isiwepo.

    ReplyDelete
  9. Teh teh teh teh,
    Mchecheto,unacheza na mwenye amri?unacheza na jeshi?
    Acha kabisa.

    ReplyDelete
  10. Nawapinga wote hapo juu.hamjui nini Chadema wanadai. Huwezi kumwambia mtu atoe mali zake. Inabidi uiambie serikali ikupe uhuru nawe ujitafutie kwa jasho lako mwenyewe. Mbowe ametoa makubwa zaidi ya pesa. Anadai haki, na uhuru kwenu nyote. Hii ni kubwa kuliko pesa za bure. Hamjajua na hamjapevuka bado kisiasa.

    ReplyDelete
  11. udikteta usaidie, Rais kabla ajapewa wenye kiti alikiwa anasikiliza ukawa wanasema nini. Baada ya kupewa wenyekiti mambo yakabadilika. kilakitu ccm,ccm,ccm.Demokrasia nikusikiliza na wapinzani wanasema nini, si lazima serekali itii.

    ReplyDelete
  12. Hivi wewe Mbowe na hao vichwa maji wenzako ni lini mtaanza kufikiria maendeleo ya wananchi waliowachagua. Tumewachokaaaaaaaa na mbinu zenu za kuvuruga amani na maendeleo zishindwe ktk jina la Yesu.....

    ReplyDelete
  13. Tuombe amani Tz, ukuta ushindwe kwa jina la Yesu, tutakwenda wapi fujo ikianza, mbowe unakimbilia dubai usichanganye watu akili.

    ReplyDelete
  14. Tuombe amani Tz, ukuta ushindwe kwa jina la Yesu, tutakwenda wapi fujo ikianza, mbowe unakimbilia dubai usichanganye watu akili.

    ReplyDelete
  15. Mbowe Mie nakuona laana za Mama Zitto zinaanza kukusibu. Maana yake hueleweki au hujielewi... Kuburi na jeuri unayo jaribu kuileta kwetu mbona inatuchanganya au unachanganyikiwa?? Hivyo wewe mara ya mwisho ulichukua Vacation lini na ukapata mapumziko ya mwili na Akili?? hebu tujulishe maana unatia huruma!! au ndiyo Magu effect? JpJM hana mchezo!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad