Majambazi 10 yateka magari, yaua dereva

Wafanyabiashara waliokuwa wakitoka mnadani wamevamiwa na majambazi yapatayo 10 ambayo na kumuua kwa risasi dereva aliyegoma kuwapa fedha na simu.

Dereva huyo, Chrispin Inyangwe (40) alipigwa risasi ya mgongoni alipojaribu kupambana nao.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana eneo la katikati ya vijiji vya Miula na Kalundi vilivyopo Kata ya Kipande wilayani Nkasi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema wafanyabiashara hao walikuwa wakitokea mnadani na walipofika eneo hilo walikuta mawe yamepangwa barabarani kuzuia magari.

Amesema baada ya kuona mawe hayo, magari hayo yalilazimika kusimama na ndipo majambazi hao waliokuwa na silaha za moto, mapanga na marungu walipoibuka na kufyatua risasi hewani na baadaye kutaka wafanyabiashara hao wasalimishe fedha na simu zao za mkononi.


Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. polisi wajitahidi..kwenye matukio ya mikusanyiko ya watu kama hii tena inayoeleweka watu wanaenda kukusanya fedha..kwa nini wananchi hawapewi ulinzi unaostahili?kulipaswa kuwe na patrol ya siku nzima maeneo hayo...daa...inasikitisha sana.tukisema sana mtatufunga....

    ReplyDelete
  2. Serikali imtayarishe kila raia kuwa mlinzi. Jeshi la polisi, jeshi la wananchi waungane na raia kutoa mafunzo. Kuwe na roll call kujua kila mtu alipo.zidisheni bituo vya usalama. Toeni vitambulishokwa kila mtu.kila mtu asiyejulikana muwe suspicious naye na aulizweau interrogated. Bunduki nyingi zinaingiaje.watu wasiruhusiwe kubeba panga.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad