Maoni ya Alberto Msando Juu ya Kauli Tata za Rais Magufuli

Sina tatizo na hatua za Raisi kuleta 'maendeleo' kwa wananchi na kutetea 'wanyonge'. ILA nina tatizo na kauli zake. Kuna jinsi ambavyo kama watanzania tumezoea kusemeshana na kuongeleshana. Sisemi kwamba tuishi kwa mazoea la hasha. Ila ni vyema mtu yeyote uangalie unasema nini na wapi kufanikiwa nini.

Mlimani City mpango wa kuijenga ulianza kipindi cha Mh. Mkapa na kumalizika kipindi cha Mh. Kikwete kama sikosei. Leo hii kusema kwamba mradi huo ni "magodown" ni kuwaonea waliokuwepo wakati unatekelezwa.

Mosi, maamuzi ya Serikali yeyote ni ya pamoja (collective responsibility). Kama mtu alikuwepo kwenye mabaraza yote ya mawaziri kipindi cha Mh. Mkapa na Mh. Kikwete kipindi ambacho magodown yamejengwa basi hawezi kuepuka ushiriki katika kudanganywa kwetu!! Pili, sijamsikia mtu akisema barabara ambazo zimebomoka (mfano maeneo ya Chalinze, barabara ya Mbeya, barabara za akachube nk) ni mitaro au mito kwa sababu zilijengwa chini ya kiwango!! Au ule mradi wa ferry kutoka Bagamoyo - Dar ni WHITE ELEPHANT. Au kukumbushia uuzaji wa nyumba za Serikali halafu kwenda kujenga nyingine!! Au kuhusu wale samaki wa wachina kwamba tuliingizwa chaka.

Tatu, uongozi ni endelevu. Zaidi pale ambapo bado ni CCM ndio kipo madarakani. Inatuchanganya wananchi tunapoambiwa tulichezewa na kudanganywa sana huko nyuma. Nyuma tunayoijua sisi ni ya NYERERE, MWINYI, MKAPA na KIKWETE. "Nyuma" ya CCM. Je ni yupi kati yao alikuwa mzembe na asiyejua kuongoza kiasi kwamba leo hii tuko hapa na magodown yetu???? Atuombe msamaha!! Kwa njia moja au nyingine ni ukweli kwamba sisi watanzania ni majuha. Tumechezewa wakati wa hao wote wala hatukujua. Leo angalau ametokea mtu kutuambia ukweli. Mzee Mkapa alikuwa sahihi kutuita malofa.

Lakini najaribu kujiamiaminisha kwamba Mh. Raisi ni mtu wa kauli za utani. Mfano, 1. Kufyatua watoto 2. Siasa mpaka 2020 3. Kuwapoteza nusu walioimba kwenye mkutano 4. Kumzamisha kisimani aliyezuia watu kuchota maji 5. Kutoa matairi kwenye magari yanayovunja sheria za barabarani 6. Polisi kutokuwa rafiki na raia 7. Kutokusaini pensheni mtu asipokupa mkono wa salamu nk nk.

Natamani sana niamini hivyo. Ni utani tu. Naomba sana iwe hivyo. #TatizoNiSisi

Alberto Msando
Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hakuna hata kauli moja iliyo tata aliyo isema rais JPM. Tatizo moja mlionalo baadhi ya watanzania hamtaki kuambiwa au kusikia mtu akisema ukweli, mnatanguliza majungu!! Mwacheni rais afanye kazi zake bila kuingiliwa na watu kama wewe ( Naomba usinielewe vibaya sina kinyongo na wewe mwandishi.) Nasikia watu wanasema eti siku hizi hakuna pesa!! Pesa zimekwenda wapi?? Mbona mshahara aujapunguzwa!!Eti rais hapendi kukoselewa,kuna muhubiri mmoja alisema eti ata Mungu anakosolewa!!! Matunda ya kazi nzuri za JPM sisi walioko ughaibuni tunayaona,mwacheni afanye kazi, mwacheni arudishe heshima ya Tanzania. Mungu ibariki Afrika, Tanzania na mpendwa rais JPM.
    JB Kalugira USA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kweli wewe ni zaidi ya bogus.

      Delete
    2. Mdau.. To Understand Magu you need to be focused and Hatred Free. Who can understand both sides of Coin. Magu in short he is a Game Changer in African leadership. Being governed By Performance and Achievement. His Micro Management skill is second to None.. Hangoji taarifa ofisini anazifata na kushudia mwenyewe.. Its a Man to work With/ Under.... Hapa ni Kazi Tuu

      Delete
    3. Wanaosema pesa hakuna ni wale waliokuwa wanakwepe kodi,wavivu,waliokuwa na makandokando ndani ya ofisi,mfano kalamu moja ya sh.200 mtu anadai kanunua sh.1200 n.k.sasa hayo mambo siku hizi hakuna kwani Magu kabana unadhani watakosa kusema hali ya pesa ngumu?Mimi niliyekuwa nategemea mshahara sioni kama kunatofauti,ni kilio cha miaka ypte kwamaba mshahara wa TZ hautoshi.Kweli JPJM kaleta heshima na sasa wote tunalia hali ngumu tukingojea dodo chini ya muarobaini.

      Delete
  2. Ukikuta watu porini Kill them!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ok,sasa wewe kill them uone cha moto.

      Delete
  3. GOOD...THAT IS CRITICAL THINKING..

    ReplyDelete
  4. Guys.. To Understand Magu you need to be focused and Hatred Free. Who can understand both sides of Coin. Magu in short he is a Game Changer in African leadership. Being governed By Performance and Achievement. His Micro Management skill is second to None.. Hangoji taarifa ofisini anazifata na kushudia mwenyewe.. Its a Man to work With/ Under.... Hapa ni Kazi Tuu

    ReplyDelete
  5. Albero Msando.. Ndiyo kwanza nakusikia. Naomba ujitambulishe!!!

    ReplyDelete
  6. Umesema kweli Kabisa
    Mawaziri na watumishi wote wahajiamini
    Maskini wanaogopa kutumbuliwa
    Ila ana vijana wake kawaweka dar
    Hawa wanaropoka na kufyatua
    Kila Leo wapo mwenye media
    Cha kushangaza hata wao wanamkandia JK mtu aliyewaweka wakaonekana na kujilkana
    Siwaelewi CCM na awamu ya Tano

    ReplyDelete
  7. Rais anaongea sana kwa kweli akitoa bomu ili analipua lingine da!!! inabidi awe anaandika hotuba zake halafu awe anazipitiaaa, ndiyo aje aongee. Maana wakati mwingine anapandisha jaziba ile mbayaa!!! kama kule znz alivyoongea hadi akaweka ihiiiii!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad