Matusi yavunja mkutano wa Obama na Rais wa Ufilipino

Rais wa Marekani Barack Obama amevunja mkutano wake na Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte,  baada ya  Rais huyo, kumwita Obama ‘Mwana wa Kahaba’

Obama awali alikuwa amesema kwamba angemuuliza kiongozi huyo maswali kuhusiana na mauaji ya kiholela ya watu wanaotuhumiwa kuhusika katika ulanguzi wa dawa za kulevya Ufilipino.

Lakini Bw Duterte, ambaye ameunga mkono mauaji hayo, alisema iwapo hilo lingefanyika: "Putang ina (mwana wa kahaba) nitakutusi katika mkutano huo."

Maafisa wa Obama wamesema badala yake kiongozi huyo sasa atakutana na Rais wa Korea Kusini.

Msemaji wa baraza la Taifa la Usalama Marekani Ned Price amewaambia wanahabari kwamba Obama atakutana na Park Geun-hye katika mkutano wa Mataifa ya Kusini Mashariki mwa bara Asia (Asean) mjini Laos, ambapo viongozi wamekusanyika kwa mkutano mkuu.

Obama, aliyetua Laos baada ya kuhudhuria mkutano wa G20 mjini Hangzhou, China, alitarajiwa kuuliza maswali kuhusu ukiukwaji wa haki za kibinadamu Ufilipino.

Lakini akiongea mjini Manila Jumatatu kabla ya kuondoka kuelekea Laos, Duterte alishutumu hilo na kusema ni "kukosa adabu" na akamtusi rais huyo wa Marekani. Aliongeza kwamba: "Tutagaragazana matopeni kama nguruwe iwapo utafanya hilo."

Kisha, alizungumzia kampeni ya kukabiliana na walanguzi wa dawa za kulevya ambapo washukiwa 2,400, wakijumuisha walanguzi na watumizi, wameuawa nchini Ufilipino tangu achukue mamlaka mwezi Juni.

"Kampeni dhidi ya dawa za kulevya itaendelea. Wengi watafariki, wengi watauawa hadi tuangamize mlanguzi wa mwisho na kumuondoa kutoka barabarani ... hadi mtengenezaji wa mwisho wa dawa hizi auawe, tutaendelea."

 Obama awali alidunisha matusi hayo na kusema aliwaomba maafisa wake kuchunguza iwapo huu ni wakati mwafaka wa kuwa na mashauriano ya kufana.

Baadaye, maafisa wake walivunjilia mbali mkutano huo.

Ziara ya mwisho ya Obama bara Asia akiwa kama rais imejaa vioja. Alipowasili Uchina, alijip kwenye mzozo wa itifaki kati ya maafisa wa Marekani na Uchina ambapo alikosa kuwekewa zulia jekundu.

Matusi

Hii si mara ya kwanza kwa Rais Duterte kutumia lugha chafu kuwarejelea viongozi mashuhuri.

Alimwita Papa Francis "mwana wa kahaba", waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Keryy "mwendawazimu" na majuzi alimweleza balozi wa Marekani nchini Ufilipino kama "mpenzi wa jinsia moja ambaye ni mwana wa kahaba".
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Oops ungekuwa Tanzania ungekoma toka kwa polisi uchwara
    Ungenyea debe hadi 2020
    Chezea Tanzania ya awamu ya Tano
    Hapa kazi tu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad