Mgogoro wa CUF Wachukua Sura Mpya..Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha Nusura Kutekwa na Wanachama

Filamu ya mgogoro wa CUF sasa imeingia hatua mpya baada ya wanachama watatu kuhojiwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kutaka kumteka mkurugenzi wa uchumi na fedha wa chama hicho, Jorah Bashange.

Chama hicho kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar kimekuwa na mgogoro wa kiungozi tangu Profesa Ibrahim Lipumba ambaye alijivua uenyekiti Julai mwaka jana, atangaze nia ya kurejea kwenye uongozi.

Katika tukio la jana linalodaiwa kutokea saa 2.30 asubuhi wakati Bashange akitoka nyumbani kwake, limeripotiwa kituo cha polisi cha Buguruni wilayani Ilala.

Kamanda wa Ilala ambayo kipolisi ni mkoa, Salum Hamduni aliiambia Mwananchi kuwa watuhumiwa hao wanahojiwa na polisi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad