Nimehudhuria Mkutano wa Ukanda Kuhusu Mkataba wa EPA, Tanzania Tumeonesha Njia

Jana wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameamua kwa pamoja kusitisha kuweka sahihi mkataba wa EPA hadi Januari mwakani. Awali, Kenya na Rwanda walikuwa wamekwisha weka sahihi mikataba hii.

Uamuzi huu unaziweka nchi za ukanda huu katika nafasi salama ya kutafakari na kupima faida na hasara za kusaini mikataba hii. Tayari Tanzania imeonesha mfano kwa kusita kuingia makubaliano hadi itakapojiridhisha kuhusu faida na hasara za mkataba huu.

Nimehudhuria mkutano wa ukanda kuhusu mkataba wa EPA Afrika Mashariki na kupata nafasi kujadili mambo haya wakati wakuu wa nchi wakiweka misimamo yao. Umekuwa wakati muafaka kwa matukio haya.

Kwa kusita kusaini na kuzishawishi nchi nyingine kusubiri, Tanzania imeonesha njia katika kusimamia mikataba ya aina hii.

Nitakuja na taarifa ndefu zaidi lakini kwa hatua hii, wenzetu toka nchi jirani wametuheshimu. Tutunze heshima hii na kuendelea kuonesha njia sahihi katika masuala ya diplomasia ya biashara
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. SWADATAAAAAAAAAAA!

    ReplyDelete
  2. Magufuli Baba.. Tumekupa nchi na Tunakuamini Sana.. Mikataba ya Ndivyo sivyo. Unaikata.. Mikataba ya Faida kwa nchi na wananchi. Unaweka Dole. Mungu akulinde. Hapa tumechukia Ubadhirifu na Tuanataka Uaminifu na Waaminifu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Watanzania hatujampa nchi
      Ila CCM kwa wizi wa kura wammempa nchi
      Rais anayetumbuwa alio wachanguwa mwenyewe
      Wengine wameishia kukaa hotel,
      Wengine hadi siku ya kuapishwa
      Wengine watapangiwa kazi nyingine
      Cha ajabu Rais anatamba na kujisifu wote waliowateuwa
      Alipitia majina Yao usiku na mchana hadi alipo wateuwa
      Oops CCM hiyo na ilani zake
      Wateuliwa wengi si dhani wana mori ya kazi


      Delete
    2. Mdau, Inadhihirisha kuwa wewe ni NDUMILAKUWILI. Sisi Wazalendo kwa uzalendo wetu Tumempa nchi kwa Imani zetu na Roho Moja. Yeye ndiye aliyeshika na Kuliongoza Jahazi letu katika Msafara wetu Huu. Dhoruba ndiyo kama nyinyi lakini Tunaimani kuwa Nahodha wetu atatuvukisha na Tutafika Salama... Pole wenzangu kaa uduwae. Ukitahamaki.......... Kumbuka Hapa ni Kazi Tu

      Delete
    3. Mpe na mama yako na mkeo
      Fyuuuuuu
      Kama anafaaa

      Delete
    4. Wewe ni Mkosefu wa Maadili.. Upuuzi kama huu hatuuvumilii.. Jiheshimu amu umeguswa sana na spidi ya JPJM. Hapa kazi tu. Wajibika na utafute Riziki ya Halali.

      Delete
    5. Wewe ni Mkosefu wa Maadili.. Upuuzi kama huu hatuuvumilii.. Jiheshimu ama umeguswa sana na spidi ya JPJM. Hapa kazi tu. Wajibika na utafute Riziki ya Halali. Kwa Uaminifu na Uzalendo.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad