Polisi Wafyatua Risasi na Mabomu ya Machozi Kuwatawanya Wafuasi wa Prof. Lipumba

Jeshi la Polisi limelazimika kufyatua risasi angani na kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Prof. Lipumba waliokuwa wakimzuia mwenyekiti wa muda wa CUF, Julius Mtatiro, kuingia ofisini eneo la Buguruni.

Wafuasi hao wameeleza kuwa wameamua kumzuia kwani Msajili wa Vyama vya Siasa ametaka shughuli zozote ndani ya CUF zisiendelee hadi hapo mgogoro wa uongozi utakapotatuliwa.

Itakumbukwa hivi karibuni CUF kilimteua Julius Sunday Mtatiro kuwa mwenyekiti wa muda baada ya mwenyekiti aliyekuwepo, Prof. Lipumba kijiuzulu Agosti 2015.

Julius Mtatiro leo amefanya mkutano na waandishi wa habari  katika ofisi za Makao Makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam ili kuzungumzia kauli zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akiwa visiwani Zanzibar.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hapo wenyewe kwa wenyewe wana vurugana na badoooo,,,,kazi yenu kuita watu Makafiri,,,sijui nyie mlio laniwaa mpewe jina gani.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad