Profesa Lipumba Asema Hana mpango wa kuhama CUF wala kuanzisha chama Kingine, Ataja Sababu Zilizomfanya Amkatae Lowassa

Aliyekuwa mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema hana mpango wa kuhamia chama chochote.

Aidha amesema hana mpango wa kuanzisha chama chake kwa kuwa yeye bado ni Mwenyekiti halali wa CUF kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho.

Akiongea katika kipindi cha Powerbreakfast cha Clouds FM Alhamisi hii, Profesa Lipumba amesema Katibu Mkuu wa CUF anataka kukiua chama cha CUF Tanzania bara.

“Mimi nipo CUF bado, na ni Mwenyekiti halali kwa mujibu wa Katiba na sina mpango wa kuhamia chama kingine,”

“Katibu Mkuu wetu anataka chama hiki upande wa bara kife kabisa na ibaki CHADEMA pekee yake ndio maana anafukuza wabunge.,”

Pia Lipumba amesema Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif alikosea kumnyima mkono Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein kwa kuwa unapoenda kwenye msiba jambo la msiba lilipaswa kutawala.

“Hata mimi nilipokutana na Maalim baada ya kunikatalia kurudi kwenye uenyekiti tulisalimiana.” Alisema Lipumba.

Katika hatua nyingine Lipumba alizungumzia sababu ya kutomkubali Mh. Edward Lowassa kuingia UKAWA.

“Sababu za msingi za kutomkubali Mh. Edward Lowassa kuingia UKAWA, ni kwamba ukiwa katika siasa unahitaji uongozwe na misingi na ‘principals’ na hoja kwamba mnagombea kitu gani, na sisi tulianzisha UKAWA kwa kusema kwamba tutafute nchi, serikali na dola inayowajibika ambayo inatengeneza mambo vizuri, inatumia rasilimali vizuri itapambana na ufisadi na itajenga demokrasia ya kweli katika nchi yetu, ukiwa na misingi hiyo kwamba utataka kiongozi ambaye anaunga mkono misingi hiyo na tulikuwa wote kwenye bunge la katiba na Mh. Edward Lowassa alikuwepo kwenye bunge hilo hakuwa mmoja ya wabunge aliyeunga mkono rasimu ya Katiba,” alisema Lipumba.

Alioongeza, “Kwahiyo ilikuwa ni kinyume kabisa na ile misingi iliyotuunganisha kwamba utataka kiongozi ambaye anaunga mkono misingi hiyo na ukumbuke Mh. Edward Lowassa alikuwepo katika bunge la katiba ya rasimu ya Jaji Warioba na hakuunga mkono rasimu hiyo kwahiyo ilikuwa ni kinyume kabisa na ile misingi iliyotuunganisha na kuanzisha UKAWA kuja kumchukua Edward Lowassa ndiye awe mgombea urais wa watu wanaounga mkono rasimu ya Jaji Warioba,”
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kumkubali Lowasa ilikuwa na uchu tu wa madaraka wakiamini UKAWA ingeshinda kwa kuwa Mh.Lowasa anakubalika na wengi na kwao ingekuwa mteremko wa kukwepa mambo mengi kama kutolipa madeni ya serikali kwani wangejigawia madaraka wenyewe kwa wenyewe.Mungu wetu aliye juu atawasambaratisha tu,na JPJM atabaki kukubalika mpaka hapo hali itakapokuwa nzuri.Tuna imani nae sana tu ni swala la muda.MUNGU IBARIKI TZ.

    ReplyDelete
  2. Prof. Binafsi nilikukubali sana pale ulipokuwa na msimamo wako wa kujitoa kwa kile ulichoamini nafsi inakusuta. Hukujali sana uhai wa chama chako wala hukutoa mwongozo kwa wafuasi wako na ukijua wazi kuwa ulikuwa mtu muhimu na mwenye wasuasi wengi sana CUF. Utusaidia prof Kama uamuzi wako ulikuwa na manufaa kwa chama cha Cuf. Najua elimu yangu ni ndogo lkn nami nitumie tu nafasi hii kukushsuri prof. Ww ni msomi mara nyingi umekuwa na hoja nzr sana za kiuchumi na umewahi kuwa mshauri wa uchumi nchi fulani na hata hapa Kwetu. Vile vile umefanya tafiti nyingi za kiuchumi. Ni vyema na ni busara kuchukua uamuzi wa kuachana na siasa hasa ktk kipindi hiki ambacho Cuf ni mshirika wa UKAWA na ww pia kunamtu humkubali ktk ukawa. Tuna mashaka Kama kweli unania ya kuimarisha upinzani au kuuzoofisha. Ni kweli uliumia sana UKAWA kukutosa ww au slaa kubeba bendera ni vyema sasa ukaishi kwa kile ulichoamini kuliko kuja na kung'ang'ania uwenyekiti. Naona unacheza ngoma ya peke yako lkn pia tayari unaanza kushangaa maalim kukataa kushikana na rais shein. Nin maanayake. Nn utakuja kukifanya. CUF Inapita wakati mgumu na aliyesababisha ni prof. Kubali kuwa ulifanya kosa kubwa waombe radhi wafuasi wa Cuf na ukawa. Nilitegemea ulipotengua uamuzi wako pia ungeomba radhi Kama ungekuwa muungwana kwa kujua kuwa uliwakuwaza wengi wakati ule.

    ReplyDelete
  3. Be carefully huyu mjamaa ni ndumi la kuwili yeye na kundi lake kuna kitu wanapika soon rather than later yote yatajitokeza jamaa zake walimwambia ajiuzulu na sasa watamrudisha kwa nguvu zote Au sivyo watakihujumu chama cha cuf kila kitu sasa wanataka iwe ni CCM tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. AbdulAziz, inapendeza sana ukitoa hoja inayotokana na utafiti wa kina juu ya jambo husika, vinginevyo utakuwa huitendei haki jamii kwa kuiambiya kile unachodhani ni sahihi wakati hujafanya utafiti juu yake.

      Delete
  4. Professor katoa sbb ss kama wewe utaki basi umetimiza demokrasia, kuhusu ndumilakuwili mbowe ndio namba moja lowassa ni sawa na kusema upinzani ni viongozi walikosa nafasi ccm

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad