RAIS Magufuli Ampa Shavu la Nguvu Aliyekuwa Mkurugfenzi wa NSSF Dr Ramadhani Dau

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 14 Septemba, 2016 amemuapisha Dkt. Ramadhani Kitwana Dau kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi, Dkt. Ramadhan Kitwana Dau alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)

Mhe. Balozi Dkt. Ramadhani Kitwana Dau anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amewaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa mitatu aliowateua mwishoni mwa wiki iliyopita.

Walioapishwa ni  kwanza, Bw. Eliya Mtinangi Ntandu anayekuwa Katibu Tawala wa kwanza wa Mkoa wa Songwe ulioanzishwa rasmi Mwezi Februari 2016.

Pili, Bw. Adoh Stephen Mapunda anayekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara.

Bw. Adoh Stephen Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Benedict Richard Ole Kuyan ambaye amestaafu.

Tatu, Bw. Tixon Tuliangine Nzunda anayekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.

Bw. Tixon Tuliangine Nzunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Symthies Emmanuel Pangisa ambaye amestaafu.

Baada ya kuapishwa, Mhe. Balozi Ramadhani Kitwana Dau na Makatibu Tawala wote watatu wamekula Kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda na kushuhudiwa na Rais Magufuli.

Matukio yote yamefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es Salaam

14 Septemba, 2016
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ramadhani Dau, Hii ni baada ya sisi kukuamini na kuona utendaji wako Bora wa kazi uliyoifanya hapo nyuma. Hili ni Jukumu ambalo leo tumekubebesha. Nia na Lengo letu ni kwamba utalitumikia Taifa kwa Roho ya Uzalendo na Uaminifu ambao Utatusaidia nchi yetu kujenga Mahusiano mema na Mazuri na Nchi uendayo kiasi kwamba Transfer of Technology na Teck Know How will be the core of your dealings na Kuweza kutuletea Wawekezaji na Kulitangaza taifa letu kwa Masilahi ya Kuliendeleza na Ikiwezekana kwa haraka ukutane na vijana wetu wanaosoma hapo na kuwakumbusha mikakati ya Ujenzi wetu wa Tanzania Mpya. Jitihada yako Tuliiona na nchi ya Malaysia tuna uhusiano mzuri na ni waelewa ajili wao si miaka mingi iliyopita walikuwa hapa tulipokuwa sisi hii leo. na wameweza kupiga hatua kubwa, Tujifunze na Tushikiane. Mungu akujaajie wepesi katika wadhifu huu tukiokiamini. Dumusha Imani yetu na Kumbuka Hapa Kazi Tu. na ni wakati wote chini ya Baba JPJM. Hongera

    ReplyDelete
  2. Rais apunguziwe madaraka viongozi wengi ni wakuteuliwa ingekuwa vizuri viongozi wawe wa kuchaguliwa na wananchi wakuu wa mikoa,wilaya hivi vyeo vingekuwa gay kuchaguliwa mawazo tuu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Viongozi wa Africa hawataki kupunguziwa madaraka ndio maana katiba mpya waliipiga chini.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad