Rais Magufuli ataka Jecha apewe Tuzo ya heshima, Amtaka Dr Shein Apunguze Upole, Watakaomsumbua Awataje Washughulikiwe

RAIS John Magufuli, amemtaka Dk. Ali Mohamed Shein, kumpa tuzo Jecha Salim, mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar, kutokana na kile alichokiita kazi nzuri aliyoifanya visiwani humo mwaka jana, kwa kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu.

Rais Magufuli aliyasema hayo jana  jioni, katika ziara yake ya kikazi visiwani Pemba. Wakati Rais Magufuli akichaguliwa katika uchaguzi wa Oktoba mwaka jana, Dk. Shein alichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar kufuatia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi mwaka huu.

“Nampongeza sana Jecha kwa kazi nzuri aliyofanya kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, na kwa kweli Dk. Shein kama kuna  tuzo zako utakazotoa, naomba usimsahau kumpa na Jecha,” alisema Rais Magufuli.

Rai Magufuli pia alimtaka Rais huyo wa Zanzibar kumtaarifu yeye ili awashughulikie watu wote wanaomsumbua visiwani humo au wanaoonekana kumzidi nguvu.

“Rais Shein kama kuna mtu unaona anakusumbua wewe au anakupa tabu nijulishe mimi tu, hata dakika tano hazitapita nitamshughulikia,” ameeleza.

Kauli hiyo inakuja, ikiwa ni zaidi ya miezi kumi sasa tangu hali ya mahusiano baina ya wananchi wa Zanzibar iwe tete, tangu pale Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi visiwani humo (ZEC) alipotangaza kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Mahusiano hayo mabaya yamesababisha, wafuasi wa vyama vya CUF na CCM vyenye nguvu zaidi visiwani humo, kufikia hatua ya kusitisha ushirikiano katika shuguli za kiuchumi na kijamii ikiwemo kutohudhuria misiba na kutonunua bidhaa za mtu wasiyeendana naye kiitikadi.

“Niombe vyombo vya ulinzi na usalama wafuatilie hao wanaokatakata na kuchoma karafuu washughulikiwe bila huruma. Atakayejaribu kuichezea amani, atacheza yeye tena mchezo asiojua kuucheza,” aling’aka Rais Magufuli.

Tangu kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka jana visiwani Zanzibar, hali ya usalama imekuwa si ya kuridhisha.

Nyumba na mashamba ya karafuu yamekuwa yakichomwa moto, huku baadhi ya watu wakitiwa mbaroni  na vyombo vya dola kwa tuhuma hizo

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Uchwara wote hao

    ReplyDelete
  2. Nasikia kutapika
    Wametutoka wote wawili
    Madikteta uchwara
    Fuck fuck fuck

    ReplyDelete
  3. Rais mzima unashabikia wizi wa kura
    Inatutia wasi wasi hata wewe uliiiba kura zetu
    Inchi haingozwi kijeshi?
    Hata mfanyeje CCM haitakuwa milele Tanzania
    Yote haya mtaja yalipa
    Mungu awalaani nyote
    Kwa uongo na unafiki

    ReplyDelete
    Replies
    1. akulaani wewe na familia yako yote, peleka maujinga yako kule mfyuuuu

      Delete
  4. Ya Tanganyika hujayamaliza na una dandandia ya Zanzibar
    Kweli Tindu anasema u kweli u dikteta uchwara na rais mpunga chuya

    ReplyDelete
  5. Inchi inaendeshwa kikatiba magufuli

    Haiendeshwi kwa utashi au uamuzi wa rais
    Inaangilia kichwani kwani upinzani wanakuita dikteta uchwara
    Kwa sisi watu wa pwani ni mtu mropkaji
    Mbavu
    Hajui asemalo
    Wala hakujui jinsi ya kuongoza
    Hafuati katiba
    Mwisho
    NI LIMBUKENI WA CHEO

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad