RAIS John Magufuli, amemtaka Dk. Ali Mohamed Shein, kumpa tuzo Jecha Salim, mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar, kutokana na kile alichokiita kazi nzuri aliyoifanya visiwani humo mwaka jana, kwa kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu, anaandika Pendo Omary.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo jioni, katika ziara yake ya kikazi visiwani Pemba. Wakati Rais Magufuli akichaguliwa katika uchaguzi wa Oktoba mwaka jana, Dk. Shein alichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar kufuatia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi mwaka huu.
“Nampongeza sana Jecha kwa kazi nzuri aliyofanya kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, na kwa kweli Dk. Shein kama tuzo zako utakazotoa, naomba usimsahau kumpa na Jecha,” amesema Rais Magufuli.
Rai Magufuli pia amemtaka Rais huyo wa Zanzibar kumta
arifu yeye ili awashughulikie watu wote wanaomsumbua visiwani humo au wanaoonekana kumzidi nguvu.
“Rais Shein kama kuna mtu unaona anakusumbua wewe au anakupa tabu nijulishe mimi tu, hata dakika tano hazitapita nitamshughulikia,” ameeleza.
Kauli hiyo inakuja, ikiwa ni zaidi ya miezi kumi sasa tangu hali ya mahusiano baina ya wananchi wa Zanzibar iwe tete, tangu pale Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi visiwani humo (ZEC) alipotangaza kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Mahusiano hayo mabaya yamesababisha, wafuasi wa vyama vya CUF na CCM vyenye nguvu zaidi visiwani humo, kufikia hatua ya kusitisha ushirikiano katika shuguli za kiuchumi na kijamii ikiwemo kutohudhuria misiba na kutonunua bidhaa za mtu wasiyeendana naye kiitikadi.
“Niombe vyombo vya ulinzi na usalama wafuatilie hao wanaokatakata na kuchoma karafuu washughulikiwe bila huruma. Atakayejaribu kuichezea amani, atacheza yeye tena mchezo asiojua kuucheza,” ameng’aka Rais Magufuli.
Tangu kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka jana visiwani Zanzibar, hali ya usalama imekuwa si ya kuridhisha.
Nyumba na mashamba ya karafuu yamekuwa yakichomwa moto, huku baadhi ya watu wakilalamikia kukamatwa na kuteswa na vikosi vya ulinzi na usalama visiwani humo.
Kauli ya leo Rais Magufuli huenda ikachochea zaidi uhasama miongoni mwa wazanzibar, kwani inaonekana kulenga zaidi kuwashughulikia wapinzani wa chama tawala pamoja na Rais Shein kuliko kutafuta suluhu na maridhiano baina ya pande hizo mbili zinazohitilafiana.
CCM hiyo apewe tunzo ya wizi
ReplyDeleteUlishasema ya Zanzibar hayakuhusu
Maraisi wa Africa wana visa !!!!!!!
CCM hiyo apewe tunzo ya wizi
ReplyDeleteUlishasema ya Zanzibar hayakuhusu
Maraisi wa Africa wana visa !!!!!!!
Bila kujali yaliyotokea Zanzibar safari ya kwanza kwenda Zanzibar anatonesha kidonda na vilio vya watu waPemba. Waliuawa bila makosa , bado muna uadui, hakuna amani. Kuna namna ya kuongea mambo , kuwa na moyo kibinadamu, ukijua hasa kati ya watu waliokusanyika wamepoteza ndugu. Anaongea na raia bila huruma, kama anaongea na jeshi kwenye uwanja wa mapambano. Kwa mtu yeyete kutokuwa sensitive na watu wa chini, na kuona cheo kinamruhusu kuua ubinadamu, hii ni vita kati ya uongozi wa juu na wazanzibari ambao bado wapo kwenye majonzi.Alisema mambo ya Zanzibar hataingilia na Wazanzibar watayatatua wenyewe .leo amekwenda amewaambia wazanzibar wamsikilize kwani yeye ni raisi. Lakini alijitoa wakati WazNzibar walopomhitaji aingilie kati. Je ndio hivi viongozi wa juu mnavyoijali nchi na watu wake.
ReplyDeleteZanzibar Fitina za nini neno likitoa mdomoni harirudi raisi kisha sema na ndio kiongozi kutoka hatoki ng'o hivyo unavyo sema ni kweli na ujumbe wa raisi hakika umekufikia sawa sawa na mpiga ngumi ukutani bora tuhamie kongo
DeleteYa Zanzibar tuachie wazanzibari
ReplyDeletewewe u rais wa tanganyika
Zanzibar haingozwi kiimla
Usichagulie kiongozi Zanzibar
Hamtambui na wala hatutompa ushirikiano wowote
Ukali wako wape watanganyika
Upole wetu tuachie wanzanzibari
Haumtambui ushirikiano gani utakaouhitaji kutoka kwako watanganyika na wazanzibar ndio raisi wetu kohoa mpaka upasuke dawa zamia meli uihame zanzibar katafute raisi wako
DeleteYa Zanzibar tuachie wazanzibari
ReplyDeletewewe u rais wa tanganyika
Zanzibar haingozwi kiimla
Usichagulie kiongozi Zanzibar
Hamtambui na wala hatutompa ushirikiano wowote
Ukali wako wape watanganyika
Upole wetu tuachie wanzanzibari
Mpe tunzo na Lubuva
ReplyDeleteTujuwe moja
Rais mzima unaropoka bila kufikiri!
Sorry hukufaa wala hufai kuwa rais
Madaraka yamekuzidi akili na maarifa
Hushauriki wala huambiliki
Umeshanza na jeuri ya kisukuma eti wewe ndo rais mwenye maamuzi yote
Mwaka jana ukiomba kura ulipiga magoti kwetu fyuuuuuuu
Chunga kauli zako unaropoka na kubwatuka bila kufikiri
Tanzania haitajengwa kwa njia yako pekee yako
Watumishi wote hawafanyi kazi vizuri
Kila kukicha unatumbua watu
Mbona majipu ya jk hujatumbua?
Tumekuchoka
Mpe tunzo na Lubuva
ReplyDeleteTujuwe moja
Rais mzima unaropoka bila kufikiri!
Sorry hukufaa wala hufai kuwa rais
Madaraka yamekuzidi akili na maarifa
Hushauriki wala huambiliki
Umeshanza na jeuri ya kisukuma eti wewe ndo rais mwenye maamuzi yote
Mwaka jana ukiomba kura ulipiga magoti kwetu fyuuuuuuu
Chunga kauli zako unaropoka na kubwatuka bila kufikiri
Tanzania haitajengwa kwa njia yako pekee yako
Watumishi wote hawafanyi kazi vizuri
Kila kukicha unatumbua watu
Mbona majipu ya jk hujatumbua?
Tumekuchoka
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteNaoogopa kuchangia nisionekane mchochezi
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteMakubwa
ReplyDeleteRais gani duniani anaropoka
Ok Mugabe mtu mzima
Kama anaona Jescha anafaa kupewa tunzo
Basi aanze na kumpa mkewe Jennet
Tunzo duniani hazitolewi kama njugu
Ndo maana yule aliyekuweka madarakani Jk kajaaa na Ph.D. Za hisani dunia nzima hakuna
Sasa anza kugawa hizo tunzo
Chonde chonde
Usisahau kugawa kwa Mrema na waliorudi upinzani
CCM kuna matatizo gani
ReplyDeleteKauli sikutegemea wala kudhania zinaweza lutolewa na rais
Uchaguzi wa Zanzibar kila mtu anajuwa kabisa si mwaka jana hata kabla ya hapo
CCM mmekuwa mkiiba kura
Hata Tanganyika last year 2015
Kila siku za mwizi arobaini
Tushamuandalia andazi la shira
ReplyDelete