Rais Magufuli Ataka Jecha Apewe Tuzo

RAIS John Magufuli, amemtaka Dk. Ali Mohamed Shein, kumpa tuzo Jecha Salim, mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar, kutokana na kile alichokiita kazi nzuri aliyoifanya visiwani humo mwaka jana, kwa kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu, anaandika Pendo Omary.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo jioni, katika ziara yake ya kikazi visiwani Pemba. Wakati Rais Magufuli akichaguliwa katika uchaguzi wa Oktoba mwaka jana, Dk. Shein alichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar kufuatia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi mwaka huu.

“Nampongeza sana Jecha kwa kazi nzuri aliyofanya kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, na kwa kweli Dk. Shein kama tuzo zako utakazotoa, naomba usimsahau kumpa na Jecha,” amesema Rais Magufuli.
Rai Magufuli pia amemtaka Rais huyo wa Zanzibar kumta
arifu yeye ili awashughulikie watu wote wanaomsumbua visiwani humo au wanaoonekana kumzidi nguvu.

“Rais Shein kama kuna mtu unaona anakusumbua wewe au anakupa tabu nijulishe mimi tu, hata dakika tano hazitapita nitamshughulikia,” ameeleza.

Kauli hiyo inakuja, ikiwa ni zaidi ya miezi kumi sasa tangu hali ya mahusiano baina ya wananchi wa Zanzibar iwe tete, tangu pale Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi visiwani humo (ZEC) alipotangaza kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Mahusiano hayo mabaya yamesababisha, wafuasi wa vyama vya CUF na CCM vyenye nguvu zaidi visiwani humo, kufikia hatua ya kusitisha ushirikiano katika shuguli za kiuchumi na kijamii ikiwemo kutohudhuria misiba na kutonunua bidhaa za mtu wasiyeendana naye kiitikadi.

“Niombe vyombo vya ulinzi na usalama wafuatilie hao wanaokatakata na kuchoma karafuu washughulikiwe bila huruma. Atakayejaribu kuichezea amani, atacheza yeye tena mchezo asiojua kuucheza,” ameng’aka Rais Magufuli.

Tangu kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka jana visiwani Zanzibar, hali ya usalama imekuwa si ya kuridhisha.

Nyumba na mashamba ya karafuu yamekuwa yakichomwa moto, huku baadhi ya watu wakilalamikia kukamatwa na kuteswa na vikosi vya ulinzi na usalama visiwani humo.

Kauli ya leo Rais Magufuli huenda ikachochea zaidi uhasama miongoni mwa wazanzibar, kwani inaonekana kulenga zaidi kuwashughulikia wapinzani wa chama tawala pamoja na Rais Shein kuliko kutafuta suluhu na maridhiano baina ya pande hizo mbili zinazohitilafiana.
Tags

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. CCM hiyo apewe tunzo ya wizi
    Ulishasema ya Zanzibar hayakuhusu
    Maraisi wa Africa wana visa !!!!!!!

    ReplyDelete
  2. CCM hiyo apewe tunzo ya wizi
    Ulishasema ya Zanzibar hayakuhusu
    Maraisi wa Africa wana visa !!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Bila kujali yaliyotokea Zanzibar safari ya kwanza kwenda Zanzibar anatonesha kidonda na vilio vya watu waPemba. Waliuawa bila makosa , bado muna uadui, hakuna amani. Kuna namna ya kuongea mambo , kuwa na moyo kibinadamu, ukijua hasa kati ya watu waliokusanyika wamepoteza ndugu. Anaongea na raia bila huruma, kama anaongea na jeshi kwenye uwanja wa mapambano. Kwa mtu yeyete kutokuwa sensitive na watu wa chini, na kuona cheo kinamruhusu kuua ubinadamu, hii ni vita kati ya uongozi wa juu na wazanzibari ambao bado wapo kwenye majonzi.Alisema mambo ya Zanzibar hataingilia na Wazanzibar watayatatua wenyewe .leo amekwenda amewaambia wazanzibar wamsikilize kwani yeye ni raisi. Lakini alijitoa wakati WazNzibar walopomhitaji aingilie kati. Je ndio hivi viongozi wa juu mnavyoijali nchi na watu wake.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Zanzibar Fitina za nini neno likitoa mdomoni harirudi raisi kisha sema na ndio kiongozi kutoka hatoki ng'o hivyo unavyo sema ni kweli na ujumbe wa raisi hakika umekufikia sawa sawa na mpiga ngumi ukutani bora tuhamie kongo

      Delete
  4. Ya Zanzibar tuachie wazanzibari
    wewe u rais wa tanganyika
    Zanzibar haingozwi kiimla
    Usichagulie kiongozi Zanzibar
    Hamtambui na wala hatutompa ushirikiano wowote
    Ukali wako wape watanganyika
    Upole wetu tuachie wanzanzibari

    ReplyDelete
    Replies
    1. Haumtambui ushirikiano gani utakaouhitaji kutoka kwako watanganyika na wazanzibar ndio raisi wetu kohoa mpaka upasuke dawa zamia meli uihame zanzibar katafute raisi wako

      Delete
  5. Ya Zanzibar tuachie wazanzibari
    wewe u rais wa tanganyika
    Zanzibar haingozwi kiimla
    Usichagulie kiongozi Zanzibar
    Hamtambui na wala hatutompa ushirikiano wowote
    Ukali wako wape watanganyika
    Upole wetu tuachie wanzanzibari

    ReplyDelete
  6. Mpe tunzo na Lubuva
    Tujuwe moja
    Rais mzima unaropoka bila kufikiri!
    Sorry hukufaa wala hufai kuwa rais
    Madaraka yamekuzidi akili na maarifa
    Hushauriki wala huambiliki
    Umeshanza na jeuri ya kisukuma eti wewe ndo rais mwenye maamuzi yote
    Mwaka jana ukiomba kura ulipiga magoti kwetu fyuuuuuuu
    Chunga kauli zako unaropoka na kubwatuka bila kufikiri
    Tanzania haitajengwa kwa njia yako pekee yako
    Watumishi wote hawafanyi kazi vizuri
    Kila kukicha unatumbua watu
    Mbona majipu ya jk hujatumbua?
    Tumekuchoka

    ReplyDelete
  7. Mpe tunzo na Lubuva
    Tujuwe moja
    Rais mzima unaropoka bila kufikiri!
    Sorry hukufaa wala hufai kuwa rais
    Madaraka yamekuzidi akili na maarifa
    Hushauriki wala huambiliki
    Umeshanza na jeuri ya kisukuma eti wewe ndo rais mwenye maamuzi yote
    Mwaka jana ukiomba kura ulipiga magoti kwetu fyuuuuuuu
    Chunga kauli zako unaropoka na kubwatuka bila kufikiri
    Tanzania haitajengwa kwa njia yako pekee yako
    Watumishi wote hawafanyi kazi vizuri
    Kila kukicha unatumbua watu
    Mbona majipu ya jk hujatumbua?
    Tumekuchoka

    ReplyDelete
  8. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  9. Naoogopa kuchangia nisionekane mchochezi

    ReplyDelete
  10. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  11. Makubwa
    Rais gani duniani anaropoka
    Ok Mugabe mtu mzima
    Kama anaona Jescha anafaa kupewa tunzo
    Basi aanze na kumpa mkewe Jennet
    Tunzo duniani hazitolewi kama njugu
    Ndo maana yule aliyekuweka madarakani Jk kajaaa na Ph.D. Za hisani dunia nzima hakuna
    Sasa anza kugawa hizo tunzo
    Chonde chonde
    Usisahau kugawa kwa Mrema na waliorudi upinzani

    ReplyDelete
  12. CCM kuna matatizo gani
    Kauli sikutegemea wala kudhania zinaweza lutolewa na rais
    Uchaguzi wa Zanzibar kila mtu anajuwa kabisa si mwaka jana hata kabla ya hapo
    CCM mmekuwa mkiiba kura
    Hata Tanganyika last year 2015
    Kila siku za mwizi arobaini

    ReplyDelete
  13. Tushamuandalia andazi la shira

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad