Show za Mr Blue Fiesta Wengi Wadai Ndio Msanii Bora wa Tanzania Kwa Sasa.....

Kwa mujibu wa Mrisho Mpoto, Harry Sameer, wamjua zaidi kama Mr Blue, anastahili kuwa msanii bora Tanzania.

Mpoto alidiriki kusema hivyo baada ya kushuhudia show ya hitmaker huyo wa ‘Mboga Saba’ akitumbuiza kwenye Fiesta mjini Shinyanga na kudai kuwa hajawahi kuona show moto kama ile.

“Naomba leo niseme kwa mara ya kwanza kwamba Mr Blue anastahili kuwa msanii bora katika nchi yetu ya Tanzania,” alisema Mpoto kwenye promo ya show hiyo iliyoruka Clouds FM.

Kwa miaka mingi Mr Blue amekuwa akisifiwa kwa uwezo mkubwa wa kutumbuiza jukwaani. Mwaka juzi wakati wa show hiyo pia, Kabayser alitajwa na waandaji wa Fiesta kuwa msanii aliyepata shangwe kuliko wote. Kipindi hicho alikuwa akihit na wimbo wake Pesa.

Kwa sasa Blue anafanya vizuri na wimbo wake ‘Mboga Saba’ aliomshirikisha Alikiba.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huu ndie msani namkubali Tanzania, na ndie alie nifany nipend bongo flaver. Namkubali huu jamaa. Tunamhitaji aje huku ulaya. Karibuni Blueeeeee.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad