Steve Nyerere Ajigamba 'Mimi Nina Majumba sio Nyumba'

Msanii mkongwe wa filamu Steve Nyerere amedai yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao wanamiliki nyumba nyingi lakini hataki kuzionyesha.

Akiongea katika kipindi cha Uhondo cha EFM Jumatano hii, Steve Nyerere amedai yeye haoni ufahari wa kuonyesha mali alizonazo kama wanavyofanya baadhi baadhi ya wasanii.

“Mimi nina majumba sio nyumba ila sitaki kuonyesha instagram,” alisema Steve Nyerere. “Pia kuna nyumba kubwa ambayo ndiyo nitaamia ikiisha, kwa sasa hivi nimepanga Mkwajuni Kinondoni na naishi na familia yangu,”

Katika hatua nyingine mwigizaji huyo amewataka watanzania kuhudhuria show yake ya ‘East African STANDUP COMEDY’ ambayo itafanyika kwa mara ya kwanza Jumamosi katika hotel ya Protea jijini Dar es salaam.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MTU HAJIKWEZI BALI HUKWEZWA"

    ReplyDelete
  2. Umetisha Steve! Hongera

    ReplyDelete
  3. HIHI anaropoka na kupayuka kama rais
    fyuuuuuuuuuu
    Kada wa CCM huyo
    midomo juu kama kunguru weusi
    fyuuuuu

    ReplyDelete
  4. huyu naye kaishiwa akalime mchicha tu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad