Taarifa hiyo ni ya uchochezi inayolenga kuliweka Taifa kwenye taharuki. Mhe. Makamu wa Rais yuko bega kwa bega na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba ya nchi ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka wananchi na Watanzania kwa ujumla kupuuza taarifa hiyo ambayo inalenga kupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Viongozi wetu.
Mwisho, Ofisi ya Makamu wa Rais inawasihi Watanzania kufanya kazi kwa bidii na wajiepushe na vitendo vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu nchini.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam
Huyo aliyeanzisha tu ndio akamatwe na kushughulikiwa haraka!
ReplyDeleteMwaka huu tutaona mengi na kusikia mengi
ReplyDeleteMkono wa maalim Seif unawatesa CCM
ReplyDeleteNa bado tafuteni kila sababu na viroja
Tumeshoka kuwa gagulo Tanganyika
Marais wote Tanganyika
Fyuuu tuacheni na kisiwa chetu
Tunajuwa ana na tuna sameheana
Hatuna jazba
Bali tuna pashana kulingana na mila zetu na desturi zetu
Tunashangaa wanaoparamia mambo
Kiswahili kigumu
Enter your comment...ila mbona barua haina kumb no signature wala muhurii!! ðŸ˜
ReplyDelete