Taarifa ya Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Kuomba Kujiuzulu..Ukweli Huu Hapa

Ofisi ya Makamu wa Rais inakanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, ameomba kujiuzulu nafasi yake na kwamba taarifa hiyo ni ya uzushi na uongo haina ukweli wowote.

Taarifa hiyo ni ya uchochezi inayolenga kuliweka Taifa kwenye taharuki.  Mhe. Makamu wa Rais yuko bega kwa bega na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba ya nchi ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka wananchi na Watanzania kwa ujumla kupuuza taarifa hiyo ambayo inalenga kupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Viongozi wetu.

Mwisho, Ofisi ya Makamu wa Rais inawasihi Watanzania kufanya kazi kwa bidii na wajiepushe na vitendo vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu nchini.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyo aliyeanzisha tu ndio akamatwe na kushughulikiwa haraka!

    ReplyDelete
  2. Mwaka huu tutaona mengi na kusikia mengi

    ReplyDelete
  3. Mkono wa maalim Seif unawatesa CCM
    Na bado tafuteni kila sababu na viroja
    Tumeshoka kuwa gagulo Tanganyika
    Marais wote Tanganyika
    Fyuuu tuacheni na kisiwa chetu
    Tunajuwa ana na tuna sameheana
    Hatuna jazba
    Bali tuna pashana kulingana na mila zetu na desturi zetu
    Tunashangaa wanaoparamia mambo
    Kiswahili kigumu

    ReplyDelete
  4. Enter your comment...ila mbona barua haina kumb no signature wala muhurii!! 😠

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad