TCRA Yadai Haipendi Kufungia vyombo vya Habari ila Sheria Inawalazimu

Mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania, TCRA, imesema haifurahii kuvifungia vyombo vya habari bali inavitaka vifuate kanuni na sheria zilizopo.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda, ameyasema hayo akiwa jijini Mbeya.

“Hatufurahii vyombo kufungwa, hatufurahii vyombo kupewa adhabu,lengo kubwa ni kuvifanya vyombo viwajibike, kwa mujibu wa sheria viwajibike pia kwa wananchi,viwajibike kwa nchi,” alisema.

“Tunasajili vyombo vingi ili viweze kusaidia, kuhamasisha, kuelimisha, na kuhabarisha wananchi sasa litakuwa halina maana,” aliongeza.

Hivi karibuni kamati hiyo ilikifungia kwa miezi mitatu kituo cha redio cha Radio 5.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mapunda, Mko sawa kabisa na mnailinda Jamii kwa Hutua hizi na Inabidi. Kwa Waelewa na wenye kuelewa!! Mporomoko wa Maadili unazibwa p[anapo hitajika. Jukumu Mnalo na Mamlaka Mmepewa na Kazi yenu inaridhisha. Asanteni na Hongereni. Hapa Kazi Tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad