TUNDU Lissu ailaza chali Jamhuri, kesi ya Dennis Wilson aliyemkashifu Rais Magufuli

TUNDU Lissu, Mwanasheria Mkuu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameiangusha Jamhuri katika kesi ya kumkashifu JPM iliyokuwa ikimuhusu Dennis Wilson

Wilson, mwanachama wa Chadema alishtakiwa na Jamhuri ya Tanzania katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa kuandika maneno ya kuudhi na kutaja jina la JPM katika mtandao wa kijamii.

Katika taarifa zilizotufikia muda huu kutoka Kisutu zinaeleza kuwa, mahakama hiyo imetupilia mbali kesi hiyo kutokana na washitaki (Jamhuri) kushindwa kufafanua uhalisi wa kifupisho JPM.

“Sababu ni hati magumashi ya mashtaka ambayo haikuwa na maelezo ya kutosheleza kwasababu watesi wetu (Jamhuri) hawakufafanua maana ya kifupisho ‘JPM’ ambaye ndiye walidai ameudhika na maneno ya Wilson.

“Mahakama imekubaliana na hoja yetu kwamba, JPM inaweza kuwa kifupisho cha Juma Pumba Maharage au majina yoyote yanayoanzia na JPM.

“Mahakama imewaelekeza washtaki kama wanataka kuendeleza vita yao basi walete hati ya mashtaka inayoeleweka,” amesema Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki.

Hata hivyo, baada ya mahakama kutupilia mbali shauri la Jamhuri, mshtakiwa (Wilson) alikamatwa tena.

“Tunawasubiria warudi tena mahakamani. Wakirudi tutaomba huyo JPM aliyeudhika na maneno ya Wilson aje atoe ushahidi wa kipi kilichomuudhi,” amesema Lissu
Tags

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwani hapa tz si inajulikana kua jpm ni nani hizo pumba na maharage yametokea wapi hacheni usenge nyie mahakimu kila siku nchi inashindwa kesi kama hamuwezi kazi nendeni mukalime

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unajuwa maana ya usenge? Umewatukana mahakimu? Haya tuone hiyo haki ya mitandao ipoje! Nina uhakika jela inakuhusu

      Delete
    2. unajua kwannwatu mtu anaweza akachora katuni imefanana hata na mkapa au hata kikwete ksha akaandka kpwete au mkwapa? au simu imeandkwa nocia, okia, sunericson? huwez kumfunga kisheria ingawa ni wazi amekusema au kunakili copy ya kampun flani. mahakama inaelewa ndo maana ikawa ivo.

      Delete
    3. Wewe kweli mpumbavu wewe hunatukana wangapi kila siku na yupi kakushitaki magufuri ni mtu wa kawaida na ni mpumbavu tu go report I said

      Delete
  2. Hahahahhhahhahhaha hatariiii...

    ReplyDelete
  3. nyie mnayesema mahakimu mmelaaniwa......mkawe wanasheria basi ili mhukumu kwa matakwa yenu kuonea watu wasio na hatia. Sheria ni majadiliano na wala sio maelekezo ya mtu au matamko......Nani kasema kirefu cha JPM ni jina flani la mtu. Acheni roho za kishetani hzo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Leo utalala kusimama wewe ...haha haha kichaa wewe .....

      Delete
  4. JPM ni rais wetu,hilo liko wazi.
    Sentence yenyewe ilivyokuwa inaonyesha kabisa alikuwa anamsema nani,(Rais),labda mahakama mtuambie kama kuna ajenda nyingine ndani yake.

    ReplyDelete
  5. Bado inanishangaza kiongozi kama Lissu anapotetea maovu.

    ReplyDelete
  6. pumba maharangeeeeeeeeeeeeeeeeeeee hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa................mamaeeeeeeeeeee nchii imevaa kitop na chupii hahaha inatembeaaa

    ReplyDelete
  7. tatizo la baadhi ya vilaza wengi Tanzania wamezoea hukumu za kiiuonevu hizo wao wanaziona ndio hukumu bora but hukumu zinazofuata sheria wao wanaziona ni za kibwege na ndio maana hatuendi mbele angalia mashehe wa muamsho hawana hatia ila tu kwa kuwafurahisha mafirauni madomo upande ndio wamewekwa ndani bila sheria yoyote. DUNIA TUNAPITA UBABE UNAMWISHO

    ReplyDelete
  8. Hivi mkiwa mmekaa sehemu halafu ukawa unasmwa bila kutajwa jina lako, si unajua kabisa nasemwa mimi? maneno aliyoyasema mshitakiwa ni dhahili alikuwa anamtukana na kumkashifu Mhe, rais JPM.Kimsingi sisi watanzania inatupasa kufikia mahali kukemea tabia mbaya za baadhi ya watu wasiostarabika ingawa wameenda shule na sina hakika na makuzi yao. Kwa Tundu Lissu kutetea maovu ni kawaida yake, hana tofauti na Majula Maghafu. Makosa yanayofanywa na watu yasipewe kipaumbele kwa kuangalia chama, ina maana Chadema inatuma watu wake kumtukana Rais wetu?je katika busara ya kawaida ya mtu mwenye akili Tundu Lissu awekwe upande gani kimaadili na tamaduni za taifa letu? hawa ndiyo wanaofanya mapenzi na watoto wao wa kike halafu akasimama mahakamani kuwa alikuwa anakula faida yake, hii je hii ni akili? kweli uenda mnaangushwa na mambo mengi, maana mnakuwa kama watoto wa mtaani kuwa amkupata malezi ya kimaadili, shame on you Chandimu.

    ReplyDelete
  9. Huyo Tundu lisu ndio kazi yake kutetea maovu, haohao alowaita mafisadi yeye ndio wakili wao, na ndio sababu wakamchukua Edo Lowasa awe raisi wao wakati haohao walimtolea povu kuwa ni fisadi, na ndio haohao walomtetea na kumpigia kampeni........hovyoooooo.....kwa mtaji huo, mtaishia kujenga UKUTA na kuubomoa wenyewe........

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad