Tundu Lissu Aishukia Serikali Kuhusu Kutumia Pesa za Mifuko ya Jamii Bila Kurudisha

*Anaandika Tundu Lissu*
Pesa za mifuko ya hifadhi ya jamii hazitajenga kiwanda chochote. Ni siasa tu.
Pesa za mifuko ya hifadhi ya umma sio pesa za serikali, ni pesa za wafanyakazi. Zinatokana na makato yao ya mishahara.

Serikali imekuwa inatumia pesa hizi kama zake, wakati sio zake. Pesa hizo zimetumika kujenga UDOM kwa makubaliano kwamba serikali hii ingerudisha pesa hizo kwa mifuko hiyo. Haijarudisha hata senti moja.

Pesa hizo zimejenga jengo la Usalama wa Taifa OysterBay Dar. Serikali haijarudisha hata senti moja kwa mifuko ilikochota pesa hizo. Pesa za mifuko zimejenga jengo la Machinga Complex Ilala Dar na nyumba za polisi Kurasini Dar. Serikali haijarudisha hata senti moja. Ndizo zilizojenga Daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni. You can rest assured haitarudi hata senti moja.

Ukweli, kama alivyosema CAG kwenye mojawapo ya taarifa zake za mwaka, mifuko ya hifadhi ya jamii ina hali mbaya ya kifedha. Hii ndio sababu wenye mamlaka wanataka kuondoa fao la kujitoa. Wameigeuza mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa shamba la bibi mpaka mifuko inakaribia kufilisika.

Sasa wanataka kuficha uchafu huu kwa blangeti la uzalendo uchwara. Wafanyakazi wa Tanzania wakikubali udanganyifu huu wataliwa kama ambavyo pesa zao zimeliwa kwenye miradi niliyoitaja.
Suala sio tuache siasa. Hatuwezi kuacha siasa. Suala ni tuache siasa za aina gani. Hawa wanasiasa wanaojivika uzalendo uchwara kuhusu hela za wafanyakazi wao wenyewe wametengenezewa utaratibu maalum ambapo wanakatwa na NSSF halafu baada ya kumaliza ubunge wanarudishiwa pesa zao. Hawasubiri wafikishe miaka sitini ndipo wapate mafao yao ya kujitoa.

Halafu wanawahubiria wafanyakazi wasubiri miaka sitini ndipo wapate mafao yao. Wana ndimi mbili kama za nyoka. Wafanyakazi wa Tanzania amkeni, hamna chochote cha kupoteza isipokuwa minyororo yenu.

Soure:Henry Kilewo
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hii ni hatari tena kubwa kama mfanykaz anakosa kaz kafukuzwa au kaamua kuacha mwenyewe hawez kupata mafao yake manayake nini huu niupumbavu mkubwa tena unyanayasajii mkubwaa..what is going on in this goverment?????????????????????????????????????? so wonderful km mbunge anapewa pesa yake akimaliza mda wake wakaz why wananchi wanyimwe pesa zao na nimakato ya mishahara yao kwa amaisha yao ya badae???????????????? mtanzania jiulize mwanaao anasoma na nini ukikosa kaz mana pesa zako za akiba serikar inazikatalia unaishije??????????????????tafakar chukua hatua acheni kushangili aupuuzi

    ReplyDelete
  2. Hiyo ndio Tz bhana.

    ReplyDelete
  3. Wstanzania wengi hawazijui sheria zao. Wengi wajinga na wavivu ws kufikiri. Ni viraza wanaokubali vitu bila kuvichunguza. Ni rahisi kushangilia maneno na vitendo vichache vya viongozi na maraisi bila kudadisi undani, athari zake, wala kutaka kujua na kutafakari.wanachangia nchi kuzorota .wakikaribishwa viubwabwa na viongozi watatulia.hawatauliza vipi hawa viongozi kujipatia uwezo wa kulishwa na di kama jufunika ukweli wa mambo.badala ya kulilia usawa, uhuru, maendeo yao wataumbuka kwa kupewa soda. Umasmini shida, umosefu wa akili janga la taifa, ujinga hautibiki.wengi watanzania bado wajinga.

    ReplyDelete
  4. Ingetuumiza sana kazi hizo pesa zingeingia ktk mifuko ya watu, kwakuwa zimetumika kwa mambo yakueleweka, hatuna-neno, ipo siku zitalipwa......lakini kwakuwa 'TUNDU' la upinzani halizibiki, kupinga ndio sera yao.............. waache wapinge

    ReplyDelete
  5. Huyu anaonekana mwenye njaa sana na mwenye roho iliyoja tamaaa,, anakujaga na mambo ya ajabu kidharau kana kwamba waTZ wote ni wajinga
    Pesa za NSSF kutumika alikokutaja ni upotoshaji,,, kwa ufupi NSSF huombwa kuwekeza pesa zake ktk miradi kama hiyo aliyoitaja bwana TAMAA
    Huyu bwana ni mpotoshaji saana na anaharibu upinzani,,,Alipotosha watu ati ehh uchumi unadorora kumbe uchumi unakuwa lakini anao wajinga wanaomkubali

    ReplyDelete
  6. inaelekea ninyi hamchangii kwenye mifuko hii. kama unachangia utajua Tundu ansema nini. hadi sasa takwimu zinasema umri wa kuishi kwa mtanzania ni miaka kati ya 45 na 50 je hizo 60 tutaikamata? nani atakula hizo pesa? ujue wengi wana kazi za kuunga unga leo miezi mitatu kesho hana kazi je atakula nini? Jamani hii sio siasa bali ni ukweli hata mh Rais analijua tena atalifanyia kazi Rais ni mtu wa nyonge kwa hiyo lazima atasimama na sisi msijipendekeze!!!!!!!!

    ReplyDelete
  7. Ni kwel kabisa unafaa kushaul hao watu rais yuko kwa ajili ya watu wanyonge kama sisi na pia fao la lakujitoa rais hajatoa neon lolote lile lakin leo anatuhumiwa kwa ajili ya fao la kujitoa achen siasa za mangengeni zilizoshiba uchu wa madaraka kama alivyo tundu lisu mchwara

    ReplyDelete
  8. always Tundu Lisu ni scam,mwongo an mnafiki anajifanya mjuaji wakati ajui kitu,kupaza sauti tu.sijui ilikuwaje mtu mwongo kama huyo akawa wakili but is days are numbered.

    ReplyDelete
  9. always Tundu Lisu ni scam,mwongo an mnafiki anajifanya mjuaji wakati ajui kitu,kupaza sauti tu.sijui ilikuwaje mtu mwongo kama huyo akawa wakili but is days are numbered.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad