Ukiamua Kukisemea Kila Kinachosikika Katika Uongozi wa Magufuli Utajitia "Stress" tu

Inahitajika nidhamu ya hali ya juu sana kifikra na kimaamuzi, kutoyumbishwa na habari zinazovuma kila kukicha katika taifa letu kwa sasa. Juzi UKUTA, jana kupatwa kwa jua, leo noti mpya kuchapishwa, kesho mtu kakamatwa kwa kumtukana Rais, hujakaa sawa mara wanafunzi hewa!

 Ukiamua kukisemea kila kinachosikika utajitia "stress" zisizo na sababu na utapoteza uelekeo. Huu ndio wakati unaohitaji kujipambanua na kujidhibiti, kwa sababu kinyume na hapo unaweza kugeuka mbwa unaehangaishwa na mifupa inayorushwa kila siku.(tena mingine kwa makusudi kukupoteza na kutafuta huruma zako). Ndio maana kwa sasa nimeamua kutohangaika kabisa na taarifa za habari hasa za kwenye TV!

 Kila siku ninashangilia maisha (huwezi kunikuta nikilalamika hata kwa bahati mbaya), kwa sababu ninajua(kwa uhakika kabisa) kwamba mabadiliko yamelifikia taifa kwa ajili ya manufaa yangu! Full stop! Mengine wanajua wenyewe wanaohusika nayo, hayanihusu!
 #SmartMind
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau, Nakusifu lisai kikubwa ni kwamba Mh. Raisi is genuine Person.. with no known prtocals or Unaweza kumtabiri. Na anonesha kuto kuwa na mihimili ya Rafiki. He potrays a straight and effective leadership unmatched. Mchezo hataki na wala hauvumilii uwe ni rafiki au kando ya pili. He Aims into an achivment leadership outspoken and full of pre warning if you do not Perform when he gives you a role.
      Umejitahidi katika kumueleza pia ndani ya hotuba zake ana break the ice kwa vichekesho.. i reality is a strong Message to the stake holders that we mean business that is not a business as usual. This is new Era Which he transform and change it completely. Magu has proved to be the ROLE MODEL IN AFRICAN LEADERSHIP. MAGU IS UNIQUE AND UNDERSTAND HIM NEEDS FOCUS AND PATIENCE.. ONLY THEN YOU CAM MARCH WITH HIM. OTHERWISE UTADUWAA NA KUSHANGAA UKITAHAMAKI MAGU AMESHASONGA MBELE NA TAIFA LINAENDELEA NA UTABAKI KUJILAUMU KWA NINI SIKUMUELEWA NA KUMPA USHIRIKIANO WANGU.. BORA TUAMKE SASA NA TUSHIRIKIANE NAE.. hAPA KAZI TU

      Delete
  2. Upuuuuzi mtupu kama unashangilia ni ww waache ambao wanachambua wachambue...nyie mnaojifanya dont care ndo hamkawii kujiua na kuacha vinoti acha habari zitolewe waelewa watasema na kuchambua...

    ReplyDelete
  3. Stress tu ipate kwa wa kuja huyu
    Ana nini fyuu
    Awape stress hao hao CCM waliomchaguwa
    Mchamba wa akili asiyejuwa kuwaza wala kufikiri
    Zanzibari ya wanzanzibari
    Tuna mila zetu na asili zetu
    Atumbuwe hao watanganyika wenzake waliompa kura za wizi
    Mkono wa Seif unamuma
    Fyuuuuu
    Na bado

    ReplyDelete
  4. Stress tu ipate kwa wa kuja huyu
    Ana nini fyuu
    Awape stress hao hao CCM waliomchaguwa
    Mchamba wa akili asiyejuwa kuwaza wala kufikiri
    Zanzibari ya wanzanzibari
    Tuna mila zetu na asili zetu
    Atumbuwe hao watanganyika wenzake waliompa kura za wizi
    Mkono wa Seif unamuma
    Fyuuuuu
    Na bado

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inaonekana JPJM kakugusa kweli,kakufungia mirija yote ya kufisadi,siku hizi baa au majumba ya starehe unaona kama mortuary,na bado usipokubali matokeo yake ndio hizo stress unazoambiwa,Hahahahahahahahah!

      Delete
  5. Ni kweli bwana na sikujua kama kuna watu kama wewe tanzania,, nawasoma wapuuzi wengi wakijiingiza au kufuatilia mambo yasiyo na maslahi ktk maisha yao hasa siasa
    Mimi kama medical doctor au engineer niliyekolifai CHADEMA au CCM na CUF havinihusu,,, Vinaowahusu ni wale tu wanaoishi ndotoni na matokeo yake ni mabaya
    Magu katufungua macho kwa kusema Hapa Kazi Tu ni kweli kama hufanyi kazi kweli utaamini kama Tanzania bila nyumba ya nyasi inawezekana bila kujiuuliza kivipi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad