Unaambiwa Uchumi wa Tanzania Umezidi Kuimarika Tangu Kuingia Kwa Serikali ya Magufuli

Mwenyekiti wa Umoja wa Maofisa Watendaji Wakuu wa Kampuni Binafsi nchini Tanzania (CEO round table), Balozi Ali Mufuruki, amesema uchumi wa Tanzania haujatetereka kama ambavyo imekuwa ikielezwa na baadhi ya watu.

Mwenyekiti wa CEO Round Table (CEOrt), Balozi Ali Mufuruki
Mufuruki amesema kuwa uchumi safari hii ndiyo umezidi kuimarika zaidi kutokana na hatua kadhaa za kiuchumi zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma za wateja wenye kipato cha juu wa benki moja jijini Dar es Salaam; Balozi Mufuruki amesema wanaotoa hoja hizo hawana ushahidi wa kisayansi kwani takwimu zinaonesha kuwa tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, mfumuko wa bei umekuwa ukishuka siku hadi siku huku thamani ya shilingi nayo ikiendelea kuimarika.

Balozi Mufuki pia amezungumzia uamuzi wa serikali kuhamishia makao yake makuu mjini Dodoma na kuitaja hatua hiyo kuwa ni fursa nyingine ya kiuchumi kwa makampuni na wafanyabiashara binafsi kwenda kuwekeza wakati huo huo jiji la Dar es Salaam likipangwa upya na kuwa kitovu cha uchumi na utalii kama ilivyo miji ya Dubai, Hong Kong, Paris na New York.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hao wanavyo hawajui jail halisi ya mtanzania wa kawaida. watu wanalala njaa. maisha hayashikiki ndugu

    ReplyDelete
  2. Ndugu ukiwa mzembe utalala sana njaa usifikiri hata kama serikali tajiri kiasi gani itakuletea sahani ya plau bure ule ushibe kazi yako ni kupiga domo vijiweni jitume kujiletea maendeleo

    ReplyDelete
  3. Muhimu sana kuona Tanzanian currency ipo stable sio iwe just temporary tu we need to see this for long time otherwise tunajipa moyo na matumaini ya ndoto tu bila Wasi Wasi inawezekana kwani ufisadi ukiondoka hapo tuna amini itawezekana kwani maradhi ya ufisadi yapo kote duniani sio Tanzania tu

    ReplyDelete
  4. Asiye-fanya-kazi-na-asile.................HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  5. Tupo na Mr President shoulder to shoulder

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad