UVCCM Wamtetea Rais Magufuli, Wasema Hotuba Yake Aliyoitoa Zanzibar Imezika upotoshaji wa siasa uchwara

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema Rais John Magufuli, hana baya alilolitamka katika mikutano yake ya Unguja na Pemba, bali amezika upotoshaji wa siasa uchwara, kusafisha upepo mchafu na kufumba vinywa vya wanasiasa wakorofi na wazushi.

Pia umetoa mwito kwa Wazanzibari kwa nguvu zote kupinga siasa chafu au zenye lengo la kuwagawa, kuwatenganisha au kuwahasimisha badala yake watambue umuhimu wa kuendeleza umoja, amani na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka alisema hayo ofisini kwake Makao Makuu ya CCM, Dodoma, alipotakiwa kueleza maoni yake kuhusu shutuma anazotupiwa Rais Magufuli ikidaiwa na baadhi ya wanasiasa kwamba alilenga kuamsha joto la mtafaruku wa kisiasa visiwani humo.

Shaka alisema hotuba ya Rais Dk Magufuli imezima siasa za uzushi na dhidi ya viongozi wanaowadanganya wafuasi wao kwamba utafanyika Uchaguzi Mkuu mwingine kabla ya mwaka 2020 na Rais Ali Mohamed Shein ataondoka madarakani ili kumpisha Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

Shaka alisema hotuba ya Rais ilikuwa yenye mashiko na maudhui, makatazo, maonyo, maelezo na wosia uliojiegemeza katika kudumisha amani nchini.

“Kuhubiri amani ni dhamana yake kiutawala, kuwaonya wananchi wanaokata mikarafuu, kutoboa mitumbwi, kufyeka mazao mashambani na wengine kukataa kuwauzia bidhaa wenzao halikuwa kosa na si jambo baya kama inavyoelezwa na wazushi wa kisiasa,” alisema Shaka.

Aidha, alisema ikiwa kuna mwanasiasa asiyemtii Rais aliye madarakani Zanzibar na hata kukataa hata mkono wake, hakuna sababu kwa kiongozi huyo kutaka msaada kwenye serikali asiyoitambua.

“Iweje baniani mbaya kiatu chake dawa, unajigamba humtambui Rais aliyeshinda na kuunda serikali ila unadoea fedha zinazokusanywa na serikali usioitambua ili usaidiwe na kulipwa marupurupu. UVCCM inaunga mkono SMZ kumnyima stahili zote hadi atakaipomtambua Rais,” alisema Shaka.

Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema wakati wa utawala wa Dk Salmin Amour Juma, Maalim Seif aliposema hamtambui kama mshindi halali hakuwa akilipwa chochote, Rais mstaafu Amani Abeid Karume hakumlipa kitu hadi alipojipeleka Ikulu Novemba 5, 2009 akatangaza kuitambua serikali yake.

Alisema matamshi ya Dk Magufuli katika hotuba zake zote, ameweka bayana kila kitu, amewakanya wanasiasa wachochezi na hatarishi kwa amani, amewaonya viongozi katika serikali zote huku akikataa uzembe, urasimu, ubadhirifu wa mali za umma na kusema wote wasiotosha, wajipime iwapo bado wanafaa au la.

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kama vijana wa CCM wataunga mkono kila ana hokizungumza mwenyekiti wao bila kufikiri basi hata wao ni mizoga.pia hawajui sheria za nc hi wala hawajui kufikiri na hawapo huru. Ni vilaza alioongelea mwenyekiti wao hapo kabla. Huwezi kuingiza siasa kwenye sheria za nchi. Ccm haimlipi huyu ni fedha za umma. Pia ukichaguliwa kiongozo ukawa na bifu binafsi na mtu hustahiri kiwa kiongozi au hujakomaa. Kumshupalia mtu mama vita ya kibinafsi ni dhambi.viongozi inabidi wafundwe namna gani wasiingize hasira binafsi kazini na kuadhibu watu. Nchi nyingi zinatoa mafunzo kwa viongozi namna ya kushiti vijambojambo.mtu unatumia muda wa kazi hadharani kimshipalia mtu wa chini yako na kuonyesha hasira na ubabe. Hii inampunguzia sifa kiongozi na kuonekana dhIfu. Unauona wazi udhaifu wake. Hiu si uongozi wenye hekima. Unapobadilisha mibao au kugeuza unawafunga watu.double standard na inakuwa uongozi wa vitisho badala ya kutumia busara. Madhara yake ni muaibika na kujiaibisha mwenyewe na kujishusha hadhi. Watu watazoeea watakusoma namba na utakuwa gumzo kila siku na uongozi hautakuwa na maendeleo sababu hata watendsji ni watafanya kazi kwa woga na si kwa mapenzi.hufundishi watu au kujenga Taifa. Unabomoa na watu watatii kama kondoo bila kujifunza lolote. Taifaa kondoo bila fikra hslina maendeleo ya kweli wala hayatadumu.ni kama au sawa na watoto wslio na baba mkali akiingia tu wananywea. Akitoka gumzo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kaka ya siasa yatakutia stress bure wenye siasa wako tuli wanakula na kushiba mwenzangu na mimi unataka yakutoe roho ni sawa na kupiga hewa ngumi jaribu kwako nyumbani uwe kiongozi bora wa watoto wako ya magafuli na seif waachie wenyewe

      Delete
  2. Huyu kijana huyu mmmh kweli shikamoo njaa yani chochote kitakachosemwa yy swa tu haangalii kuna katiba kuna sheria..ni kuropoka tu kisa katibu sijui nn wa nn...yani nakuchukia we kijana..japo mi ni kijana mwenzio ila sio kila jambo lazima uongee mengine jifunze kunyamaza...na sio kila swali lazima ujibu khaa unatia kichefu chefu

    ReplyDelete
  3. NJAA NI KITU KIBAYA SANA..BE ROYAL TO YOUR COUNTRY..KIJANA HAJITAMBUI..FYUUU

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad